JUVENTUS inapanga kuwatoa mshambuliaji wa Wales Aaron Ramsey, 29, na wa Ufaransa Adrien Rabiot, 24, kwa Manchester United kama sehemu ya kitita cha £125m ili kujaribu kumrejesha mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba 26. (La Gazzetta dello Sport, via Mail on Sunday)
Ajenti wa Pogba, Mino Raiola, amesema kwamba alifanya mazungumzo na Juventus kuhusu mchezaji huyo na kuna uwezekano wa kuondoka Manchester United msimu ujao. (Sunday Telegraph)
Manchester United inataka kumuuza Pogba kwa £100m kabla ya michuano ya Euro 2020 ili kupata pesa za kufikia wanaowalenga dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Sunday Mirror)
Manchester United inataka kumuuza Pogba kwa £100m kabla ya michuano ya Euro 2020 ili kupata pesa za kufikia wanaowalenga dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Sunday Mirror)
Wachezaji wa Manchester City waliitwa katika mkutano na mkuu wa klabu hiyo Ferran Soriano Jumamosi, saa moja baada ya klabu hiyo kupigwa marufuku ya kushiriki kombe la ligi ya mabingwa kwa misimu miwili.(Sunday Telegraph)
Aliyekuwa meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anaweza kuchukuwa nafasi ya kocha wa Manchester City Pep Guardiola iwapo raia huyo wa Uhispania ataamua kuondoka klabu hiyo. (Sun on Sunday)
Tottenham ingekuwa imemsajili wa Uingereza mshambuliaji Jack Grealish, 24, kwa £6m miezi 18 iliyopita lakini mwenyekiti Daniel Levy alikata kufikia makubaliano hao. (Sun)
Hatma ya maneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer iko mashakani baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji watatu waliokuwa walengwa katika kipindi cha usajili cha Januari. (Star Sunday)
Meneja wa Inter Milan Antonio Conte ameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sunday Mirror)
Inter Milan itamruhusu mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kujiunga na Barcelona iwapo itafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 28. (Tuttosport, via Sunday Express)
Liverpool ipo katika mazungumzo ya mwisho mwisho a kumsajili RB Leipzigstriker Timo Werner, ikiwa na nia ya kufikia kiasi cha £48m kwa mchezaji huyo wa Ujerumani (Nicolo Schira, via Sunday Express)
Mchezaji wa Arsenal Kieran Tierney analengwa na meneja wa Leicester City Brendan Rodgers, ambaye aliwahi kuwa na mchezaji huyo wa Scotland, 22, wakati akiwa Celtic. (90min)
-BBC
No comments:
Post a Comment