Wananchi wakiendelea kuchukua miche ya miti kutoka Tarafa ya Nne ya Shamba la Miti SaoHill - Mgololo.
NA FREDY MGUNDA,SAO HILL.
ZAIDI ya miche milioni moja
imegawiwa kwa wananchi wa vijiji vinavyolizunguka shamba la Miti SaoHill katika
musimu wa mwaka wa 2019/2020 kwa lengo la kuimalisha ujirani mwema ambao
umekuwa umedumu kwa miaka mingi.
Zoezi la ugawaji miche ya miti
kwa ajili ya ujirani mwema hufanyika kila mwaka kipindi cha masika kwa lengo la
kuhakikisha wanapanda miti hiyo na inakuwa kwa wakati,hasa kipindi hiki kizuri
cha mvua za msimu.
Hatua ya ugawaji wa miche ya miti
husaidia kwa kiasi kikubwa kuwakumbusha wananchi juu ya uhifadhi wa misitu
katika maeneo yao kwani wanapochukua miche hiyo huelekezwa namna na ya kuipanda
na tunzaji wake.
Hata hivyo wananchi wameendelea
kuhimizwa juu ya utunzaji wa miti wanayoipanda ili iwe na manufaa kwao na
vizazi vijavyo.
Shamba la Miti SaoHill ni
miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali yanayosimamiwa na
Wakala wa Huduma wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) lenye ukubwa wa hekta
135,903 ambazo zimehifadhiwa kwaajili ya upandaji miti kibiashara na hifadhi ya
mazingira na vyanzo vya maji,makazi ya watumishi na uwekezaji.
No comments:
Post a Comment