RC HAPI: TAKUKURU CHUNGUZENI KAMPUNI YA MWENGA HYDRO. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 27 February 2020

RC HAPI: TAKUKURU CHUNGUZENI KAMPUNI YA MWENGA HYDRO.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akitoa maagizo kwa TAKUKURU kuhusu kampuni ya Mwenga Hydro iliyopo katika wilaya ya Mufindi

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Iringa imeagizwa kuichunguza kampuni binafsi ya usambazaji wa Umeme ya Mwenga hydro power ya wilayani Mufindi kutokana na uwepo wa Taarifa za kutoza wananchi gharama zaidi ya Elfu 50 hadi 180 tofauti na bei elekezi ya shirilingi elfu 27 ili kuingiziwa Umeme.
Agizo hilo limtolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi wakai wa ziara yake ya Iringa mpya awamu ya pili Katika Tarafa ya Kibengu  yenye lengo la kukagua miradi ya Maji inayotekelezwa na  serikali, Mkuu huyo wa Mkoa akabaini kuwepo wa vitendo hivyo vya ongezeko la gharama za kuingiziwa umeme na kuiagiza (TAKUKURU) kufanya Uchunguzi na kuchukua hatua.
Hapi alisema kuwa hairuhusiwi kwa mwananchi yeyeto yule kuingiza nishati ya umeme kwa zaidi ya elfu 27,000 kwa kuwa ndio maagizo ya serikali na wizara husika hivyo hiyo habari ya wananchi kulipa kiasi kikubwa kuingiza umeme.
“Takukuru anzeni mara moja kuichunguza kampuni hiyo ya Mwenga Hidro mara moja kwa kupitia nyaraka zote muhimu ili kubaini nini kinaendelea huko” alisema Hapi

Hapi akahoji maelekezo yanayompa mamlaka ya Mwekezaji huyo kutoza Zaidi ya bei za serikali ametoa wapi hiyo mamlaka kwa kuwa serikali haijatangaza kuwa bei ya kuingiza nishati ya umeme kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo.
“Serikali imepanga bei elekezi nchi nzima hivyo hata mkoani kwangu sihitaji kusikia kitu kama hicho na takukuru mkibaini wamefanya makosa kamata weka ndani wote ambao wanausika na hujuma hiyo” alisema
 Na haya ndiyo majibu ya Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo Lydia Emmanuel akaeleza juu ya namna wanavyofanya kazi ya usambazaji wa umeme vijijini nje ya wakala wa Usambazaji Umeme vijijini REA.
Kwa upande wake meneja uzalishaji wa kampuni ya Mwenga Hidro Lydia Emmanuel alisema kuwa wamepewa vijiji 32 kwa ajili ya kuingiza umeme kwenye vijiji hivyo lakini bado kampuni hiyo inamamlaka ya kujipangia bei kwa kuwa ni kampuni binafsi.
“Kampuni yetu ilipewa leseni ya kuingiza umeme mwaka 2011 katika maeneo ambayo TANESCO haifanyi kazi hivyo kampuni hiyo imekuwa imekuwa inafanya kazi toka mwaka huo hadi leo kwa gharama hizo” alisema
Naye kaimu meneja wa Shirika la Umeme TANESCO Wilaya ya Mufindi Pascal Nayo, alisema kuwa serikali ya awamu ya tano na zilizopita zilipita ziliagiza kuwa wananchi wote wanatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 27000 tu.
Katika ziara hiyo wito umetolewa kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji ili kufanya upatikanaji wa maji kuwa endelevu katika maeneo yao hiyo ni kutokana na wadau wa Maendeleo kuwekeza miradi ya maji katika maeneo yao

No comments:

Post a Comment