JE, WAJUA KUENDESHA GARI MWENDO MDOGO NALO NI KOSA KISHERIA? - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 13 February 2020

JE, WAJUA KUENDESHA GARI MWENDO MDOGO NALO NI KOSA KISHERIA?

Kuendesha gari mwendo mdogo.

> KIFUNGU cha 56 cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 kinasema “dereva wa gari au tela ambaye bila sababu za msingi ataendesha kwa mwendo mdogo (low speed) ambao utaelekea kuwasababishia watumiaji wengine wa barabara usumbufu au utawasababishia usumbufu, atakuwa ametenda kosa na panapo hatia yake atatakiwa kuadhibiwa kwa kulipa faini”

> Sababu za msingi zaweza kuwa foleni kubwa, unaendesha ndani ya msafara rasmi , maelekezo ya vibao, ubovu wa barabara , barabara imezuiwa na waandamanaji au halaiki

> Ubovu wa gari si sababu ya kutembea taratibu. Sheria hii inaelekeza gari likiwa bovu kutokuendeshwa barabarani kwa maana ya kuwekwa pembeni ili kulirekebisha au kutafuta namna nyingine.

No comments:

Post a Comment