MWILI wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi umewasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.
Wakenya kutoka matabaka mbalimbali tayari wameanza kuutazama mwili huo wa kiongozi huyo wa zamani .
Hatua hiyo inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta aliewasili kutoka nchini Marekani mapema leo kuwa mtu wa kwanza kuutazama mwili huo.
Uhuru alipokewa na naibu wake wa rais William Ruto na mkuu wa majeshi Samson Mwathethe huku usalama ukiimarishwa.
Ruto aliwasili katika majengo ya bunge mwendo wa saa tatu na dakika 50 akiandamana na maafisa wa serikali.
Kwa sasa viongozi mbalimbali wanautazama mwili huo.
Msafara wa gari lililokuwa likiusafirisha miwli huo kutoka chumba cha Lee ulipitia barabara ya alley Road na kuingia Kenyatta Avenue kabla ya kuingia katika barabara ya bunge ambapo gwaride la
kijeshi lilifanywa kutoa heshima.
Moi ambaye aliaga dunia siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 95 atazikwa nyumbani kwake huko kabarak katika kaunti ya Nakuru tarehe 12 mwezi Februari.
Serikali ilitangaza siku ya Jumanne tarehe 11 mwezi Februari kuwa siku kuu kwa raia kushiriki katika ibada ya mazishi ya mwili wa kiongozi huyo wa zamani.
Kwa sasa wananchi waliopanga milolongo mirefu wamepewa fursa kuutaza mwili huo .Shuguli ya kuutazama mwili huo itafanyika kwa siku tatu hadi lkufikia Jumatatu.
Tangazo kutoka Ikulu lilisema kuwa mzee Moi, hata baada ya kuondoka madarakani aliendelea kulitumikia taifa la Kenya na Afrika kwa kuwafundisha viongozi wa Kenya na nje ya Kenya, akiendelea kushiriki kwenye maendeleo ya miradi mbalimbali na kazi za misaada akiihubiri amani, upendo na umoja barani Afrika na duniani.
Mzee Moi aliiongoza Kenya kuelekea kurudisha mfumo wa vyama vingi na katika vipindi vingine vingi vya changamoto; na kumalizika kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa amani mwezi Desemba mwaka 2002, wakati huo mchakato ambao ulikuwa nadra kufanyika Afrika, ambao uliweka mfano barani afrika na nje ya bara tangu wakati huo.
''Hiba yake inaishi Kenya hata leo. Filosofia ya Nyayo kuhusu 'amani, upendo na umoja' ilikuwa wimbo wake kipindi chake kama kiongozi wa nchi na serikali''. Ilieleza taarifa ya Ikulu.
-BBC
No comments:
Post a Comment