Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri akiwa na balozi Maziwa ya Asas Nick Reynolds 'Bongo Zozo' wakizungumza na wandishi wa habari mkoani Iringa,mara baada ya kumtangaza rasmi Bongozozo kuwa balozi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri akiwa na balozi Maziwa ya AsasNick Reynolds 'Bongo Zozo' wakizungumza na wandishi wa habari mkoani Iringa,mara baada ya kumtangaza rasmi Bongozozo kuwa balozi wa kampuni hiyo.
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
BALOZI
wa kampuni ya Maziwa ya Asas amewataka watanzania kunywa maziwa bora
yanayozalishwa na kampuni ya maziwa ya Asas iliyopo mkoani Iringa kwakuwa
wamekidhi vigezo vyote ya kimataifa.
Akizungumza
na vyombo vya habari Nick Reynolds 'Bongo Zozo' alisema kuwa watanzania
wanatakiwa kutumia maziwa bora ambayo yanatengenezwa hapa nchini hasa na kampuni
hii ya Asas hasa kwa wale wanamichezo hivyo hata akiwa viwanjani ataendelea kuitangaza
bidhaa ya asas kutokana na ubora wake.
SHABIKI
aliyejizoelea umaarufu wa soka nchini hivi karibuni, Nick Reynolds 'Bongo Zozo'
anatarajia kuwaongoza maelfu wa mashabiki mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo
kati ya Lipuli na Simba na kuwataka mashabiki wa soka mkoani Iringa kujitokeza
kwa wingi kuiunga mkono timu ya Lipuli Fc’ Wanapaluhengo katika mchezo wake
dhidi ya Simba unaochezwa leo katika dimba la Samora
“Nitakuwa uwanjani nakunywa maziwa ya Asas
huku nikihamasisha mashabiki kunywa maziwa ya Asas na kuipenda timu yao ya
nyumbani kama Lipuli hivyo nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya kesho
kwenye mchezo wa simba na Lipuli” alisema bongozozo
Alisema
kuwa amekaa Iringa miaka 13 hali inayomfanya kuipenda zaidi Lipuli Fc timu
ambao imekuwa ikifanya vyema dhidi ya vigogo hao na kuwataka mashabiki
kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Samora leo kwani atakuwepo uwanjani.
Alisema
mashabiki watakaojitokeza siku ya leo atahakikisha anatoa zawadi ya jezi za
Lipuli na atakaa jukwaa la mashabiki wa kawaida kufanya fujo isiyoumiza kama
ilivyoada ya kushangilia timu ya Taifa kila inaposhiriki mashindano mbalimbali
ndani na nje ya nchi.
“Nimekuja
Iringa kuhakikisha tunashangilia wanapaluhengo hivyo tujitokeze kwa wingi leo
katika mechi yetu dhidi ya Simba tuweze kuibuka na ushindi na mashabiki waje
kushuhudia fujo zisizoumiza ambapo nitakaa kwenye jukwaa la mashabiki wa
kawaida na kugawa jezi” alisema
Bongozozo
ambaye amekuja katika mchezo huo kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya Asas
aliwataka mashabiki kutumia maziwa ya Asas pindi wanaposhangilia kwani wanapata
nguvu za kushangilia bila kuchoka kutokana na ubora wa maziwa hayo nchini.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maziwa ya Asas, Ahmed Salim Abri alisema kuwa
kampuni ya Asas imeamua kufanya kazi na Bongozozo kwa kuwa amekuwa mmoja wa
mabalozi wazuri wa soka nchini hivyo wanajisikia faraja kufanya kazi naye kwani
atasaidia kutangaza bidhaa zao za maziwa ndani na nje ya nchi.
“Huyu
ni balozi wetu mpya wa bidhaa za maziwa ya ASAS. Na huu ni sehemu ya mkakati
wetu wa kuwahamasisha watanzania kunywa maziwa kwa wingi kwani kila mtu
anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka hivyo Bongo zozo atasaidia sana
katika kampeni hii” alisema.
Alisema
kwa mujibu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) mtu mmoja anatakiwa kunywa wastani wa
lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini takwimu za hapa nchini zinaonesha unywaji
wa maziwa hayo upo chini ya asilimia 40 hali inayolazimu kuwatumia watu maarufu
kuhamasisha watu wanywe maziwa zaidi hasa kutoka kampuni ya Asas.
Alisema
kuwa kwa upande wa kampuni hiyo mstari wa mbele katika kudhamini michezo
mbalimbali inayofanyika ndani ya Iringa na nje ya Iringa ikiwemo kuidhamini
timu ya Lipuli na ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa ambapo wamedhamini
kwa miaka 3.
No comments:
Post a Comment