ATCL YAZINDUA OFISI ZAKE MPYA MAFAO HOUSE JIJINI ARUSHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 1 February 2020

ATCL YAZINDUA OFISI ZAKE MPYA MAFAO HOUSE JIJINI ARUSHA



Na Ahmed Mahmoud Arusha
WATANZANIA wametakiwa kupenda na kutangaza vitu mbali mbali ambavyo vinazalishwa hapa nchini kwa lengo la kusaidia kuonyesha Uzalendo kwa Taifa.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Ofisi ya shirika la Ndege la Tanzania ATCL Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwenye hafla iliofanyika kwenye Jengo la Mafao house jijini Arusha alisema kuwa Uzalendo ni jambo jema na linahitaji Sana kwa watanzania kuitangaza shirika hilo na kuliunga mkono.

Alisema kujivunia uwepo wa shirika hilo ambalo linaitangaza Tanzania kote linapoenda sanjari na kuongeza watalii wanaokuja kuitembelea nchi yetu hivyo kuongeza pato la taifa.

Aliipongeza Bodi ya wakurugenzi wa shirika la Ndege kwa kazi nzuri ya kuendelea kuliboresha shirika hilo na kuwaomba watanzania kulipenda na kujivunia shirika hilo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo mhandisi Emmanuel Koroso alisema kuwa shirika limejipanga kuhakikisha linaenda na hadhi ya shirika la Ndege nchini ndio maana wakafungua ofisi hizo zinazoendana na hadhi ya shirika hilo.

Alisema shirika hilo limeamua kuendana na mageuzi makubwa ya kiundeshaji kuendana na kuhakikisha shirika hilo linaenda na malengo na matarajio ya serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli kuwa shirika Bora lenye kuchangia kukuza uchumi wa watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika hilo Ladslaus Matindi alisema ofisi hiyo itahudumia na kusimamia pia Ofisi za mkoa wa Kilimanjaro ambapo aliwataka watanzania kutumia usafiri huo kwa sasà wanafika katika mikoa 10 nchini lengo likiwa kufikia mikoa yote.

No comments:

Post a Comment