Watoto waishio katika mazingira hatarishi kutoka Kituo cha Safina mkoani Singida wakifurahia jambo pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya SPRF muda mfupi baada ya kupata chakula kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya Taasisi hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya SPRF, Issa Hassan (kulia) akiteta jambo na Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya SPRF, Dkt. Suleiman Muttani, akizungumza jambo na Katibu wa Taasisi hiyo Dkt. Mwajuma Ulaya na Mwenyekiti wa Sauti ya Mwanamke Kijiji cha Kipumbwiko Mwajuma Suleiman kwenye moja ya shughuli za maadhimisho hayo.
Afisa Takwimu wa SPRF, Boniventure Kagenzi akiteta jambo na muuguzi wa hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo jana.
Afisa Ufuatiliaji wa SPRF, Mwedinuhu Beleko, akiteta jambo na muuguzi wa hospitali ya Rufaa Mandewa kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi hiyo.
Katibu wa Taasisi ya SPRF, Dkt Mwajuma Ulaya akizungumza na watoto wa kituo cha watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu cha Safina (hawapo pichani). Kushoto ni Mwanasheria wa taasisi hiyo, Paul Kigeje.
Mkurugenzi wa SPRF, Dkt Suleiman Muttani akikabidhi zawadi ya taulo za kijani ambazo zinaaminika kuwa salama zaidi kwa matumizi ya watoto wachanga badala kutumia nguo za mama. Zoezi hilo lilifanyika ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani hapa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 ya SPRF.
TAASISI isiyo ya kiserikali ya Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) hatimaye imeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake huku ikitekeleza kwa vitendo malengo endelevu ya maendeleo kitaifa na kidunia sambamba na kujenga dhamira yenye taswira chanya kwa jamii, hususan uhamasishaji wa kina dhidi ukatili wa kijinsia kwa mwanamke na mtoto wa kike.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi ya taulo za kijani kwa ajili ya kuwafunika watoto waliozaliwa kabla ya umri‘ njiti,’ ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mandewa mkoani hapa jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo DkSuleimani Muttani alisema azma iliyopo ni kuendelea kusaidiana na serikali kutekeleza Mkukuta kama suluhisho la gharama za umaskini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo DkSuleimani Muttani alisema azma iliyopo ni kuendelea kusaidiana na serikali kutekeleza Mkukuta kama suluhisho la gharama za umaskini
SPRF ilipata pia nafasi ya kujumuika na kupata chakula cha mchana na watoto yatima na waishio kwenye mazingira hatarishi wa kituo cha Safina mkoani hapa kabla ya kuanza hafla ya maadhimisho hayo yaliyokutanisha viongozi mbalimbali wa dini, jamii na serikali, wakiwemo watu mashuhuri.
“Tunawashukuru SPRF kwa kutukumbuka na kutenga muda wao kuja kula chakula cha mchana pamoja nasi, Mwenyezi Mungu awabariki sana…mana wengine ni matajiri na wana uwezo lakini huwa hawatukumbuki,” alisema Ndahani Julius, mmoja wa watoto wanaotoka kituo cha watoto yatima cha Safina mkoani hapa.
Muttani alisema Malengo mengine ya taasisi hiyo, ambayo miradi yake ipo chini ya ufadhili wa Foundation for Civil Society (FCS), ni kukuza ushirikiano miongoni mwa wadau na jamii, taasisi za kitaifa na kimataifa katika kutokomeza umaskini wa kipato nchini na kwingineko, sambamba na kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika kukua na kutekeleza program endelevu.
Shirika hilo tangu kuanzishwa kwake Desemba mwaka 2014, likihamisha makao yake kutoka Dar es Salaam hadi Singida, kwa nyakati tofauti mpaka sasa limefanikiwa kuanzisha Kliniki ya akinamama inayojulikana kama Pride, mradi wa kufuga kuku.
Kindai sambamba na kutekeleza mradi wa Aware unaoendelea kufanya vizuri mpaka sasa kwenye kata 5 ndani ya wilaya yaIkungi
Kindai sambamba na kutekeleza mradi wa Aware unaoendelea kufanya vizuri mpaka sasa kwenye kata 5 ndani ya wilaya yaIkungi
“ESPRF na jamii ndio moto wetu, mradi huu wa aware umesaidia sana kumfanya mwanamke kutambua haki zake, lakini madhara ya mila zilizopitwa na wakati, masuala ya ukeketaji na mimba na ndoa utotoni ndani ya jamii,” alisema.
Muttani alisema pia shirika hilo limefanikiwa kuanzisha Kamati kwenye vijiji 8 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto huku wakihamasisha uanzishwaji wa vikundi mathalani Sauti ya Mwanamke na Sauti ya Mwanafunzi kulingana na makundi rika, vikundi ambavyo vimekuwa chachu ya mageuzi ya kifikra dhidi ya mila potofu na masuala ya ukatili ndani ya jamii
Alisema ili kuyapa nguvu mashirika yasiyo ya kiserikali kutimiza majukumu yake ipasavyo, anatamani kuona serikali kupitia bajeti yake inatenga walau asilimia moja au mbili ya bajeti ili kusadia mashirika hayo.
Mkurugenzi huyo aliitaka jamii ya watanzania kuwa na tabia ya kuzichangia asasi hizo ili kuzipa nguvu na hamasa kuweza kufanya kazi zake ipasavyo.
Kwa upande wake, Afisa Ufatiliaji wa SPRF, Mwedinuhu Beleko alisema tatizo la ukatili wa kijinsia hasa ukeketaji ni changamoto kubwa ndani ya mkoa wa Singida, baadhi ya watu bado wanafanya kwa siri na hasa nyakati za usiku wa manane.
“Nichukue nafasi hii kuwasihi sana viongozi wa kimila, wazazi, viongozi wa dini, Jeshi la Polisi na jamii kwa ujumla tushikamane ili kwa pamoja tuweze kutokomeza vitendo vya ukeketaji,” alisema Beleko.
Beleko alisema pamoja na mambo mengine, maadhimisho hayo yanatoa fursa ya wao kujitathmini kujua walipotoka, walipo na wanapoelekea katika mtazamo wa kuona jamii inakuwa na uelewa mpana hasa kwenye masuala ya ukatili wa kijinsia na namna bora ya kukabiliana na umaskini wa kipato.
Aidha, Muttani akizungumzia miaka minne ya RaisMagufuli, pamoja na kumpongeza lakini amemsihi azitazame taasisi za kiraia kama vyombo vyenye jukumu muhimu kwa taifa na kwamba zinafika mbali zaidi ambapo wakati mwingine serikali haiwezi kufika.
Tunafanya kazi ya aina moja hakuna uadui, na ni dhahiri asasi hizi zinalipa kodi kwa taifa hivyo zinapaswa kutazamwa kwa jicho la kipekee kama chachu ya mabadiliko na chanzo cha maendeleo ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment