WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YANG’ARA UANDAAJI WA RIPOTI BORA ZA MAHESABU KWA MWAKA 2018 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 8 December 2019

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YANG’ARA UANDAAJI WA RIPOTI BORA ZA MAHESABU KWA MWAKA 2018


Na Ramadhani Kissimba, Dar es Salaam

WIZARA ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imepata tuzo ya uandaaji bora wa mahesabu (Finacial statements) kwa mwaka 2018, kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu serikalini (IPSAS).

Tuzo hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban, wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wahasibu uliyofanyika Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo

Mkutano huo wa siku tatu uliowashirikisha wataalamu wa fani ya uhasibu zaidi ya 2,500 kutoka Serikali Kuu, Taasisi za Serikali, Halmashauri na Sekta Binafsi za hapa nchini pamoja na nchi za Kenya, Uganda,Burundi na Zambia, ulikuwa na lengo la kubadilishana uzoefu kwa wataalmu hao kulingana na mabadiliko ya  sekta hiyo yanayotokea ulimwenguni.

Aidha, Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwawezesha wataalam hao kuwa na lugha ya pamoja katika uaandaaji wa hesabu unaozingatia viwango vya kimataifa.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Fungu 50 Bw. Christopher Mkupama alisema Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 50 imekuwa ikifanya vizuri katika uaandaji wa hesabu za mwaka kwa kipindi cha miaka minne mfufulizo na kupelekea kupatikana kwa tuzo hizo.

Alisema kuwa Tuzo hizo zimekuwa zikiiletea sifa Wizara ya Fedha na Mipango hasa Fungu 50 na kuchochea morali ya ufanyaji kazi kwa watumishi wa fani ya uhasibu.

‘’Nawashukuru sana viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na watumishi wa Kitengo cha uhasibu kwa kutufanya tuwe washindi wa pili kwa mara nyingine katika uaandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2018, tuzo hii ni shukrani kwa watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa mchango mkubwa wanaotoa kwa wahasibu katika uandaaji wa taarifa za hesabu za kila mwaka’’ alisema Bw.Mkupama.

Mkutano wa mwaka wa wahasibu ulianza tarehe 5 hadi 7 Disemba,2019 kwa kufunguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), Bw. Charles Kichere kwa niamba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpnago (Mb) na kufungwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.

No comments:

Post a Comment