WANAFUNZI 400 WANACHANGAMOTO YA KUJINGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI MIRERANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 3 December 2019

WANAFUNZI 400 WANACHANGAMOTO YA KUJINGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI MIRERANI


Na Ahmed Mahmoud, Mererani
WANAFUNZI zaidi ya 400 wapo hatarini kutokujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa unaozikabili shule mbili za Sekondari  Benjamini Mkapa na Tanzanite zilizopo katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Kwa Muktadha huo Ofisi ya madini imewataka Wachimbaji,madalali na wafanyabiashara wa madini kuahakikisha wanarudisha kile wanachovuna kwa  kuchangia maendeleo ya jamii kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10 ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwakani.
Akizungumza katika kikao cha wachimbaji, Madalali na wafanyabiashara Jana Afisa madini Mererani, Daud Ntalimwa alisema sheria ya mwaka 2017 kifungu 105 na 106 kinawataka wafanyabiashara, madalali na wachimbaji kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo shule ili kupunguza idadi ya wanafunzi kukosa madarasa na madawati.

Alisema kuwa jumla ya million 200 zinahitaji kufanikisha ujenzi huo wa madarasa ili wanafunzi mia nne wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwakani tunatoa siku 20 kuanzia leo Dec.2.

"Mchango huu utabadilisha mtazamo wetu kuwa eneo letu ni la watu wakorofi na serikali kuona ni wadau muhimu sana kwa siku za usoni itakuwa nchi imeshawatambua na hii itakuwa mara ya kwanza kuchangia na kurudisha kwa jamii kile mnachipata kwa mujibu wa sheria," alisema Ntalimwa.

Alisema kuwa fedha hizo wanazochanga zitaisadia jamii bila kujali chochote hivyo wajibu wao ni kujitoa kwa moyo mkubwa kuweza kufanikiwa ili jamii iliyowazunguka ipate mafanikio kwa kile wanachovuna.

Alieleza kuwa jumla ya fedha zitakazopatikana baada ya kuchangisha ni takribani milion 161 ikiwa wafadhili 400 watoa takribani million 1 ambapo madalali 410 watatoa 100,000 kila moja wachimbaji 50 watoa 500,000 kila kampuni.

Awali akiongea Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Kilempu Laizer alisema kutokana na ufaulu wa watoto 700 wa Merelani kuongezeka kwa mwaka huu hivyo na upungufu wa madarasa hupo kwa shule hizo hivyo tukaomba wananchi na wadau wa madini tushirikiane kujenga madarasa na madawati ili watoto wasiteseke kwa kukaa chini.

"Watoto wa merelani wanateseka sana  kuhusu swala la elimu hivyo tukaomba kila mtu na nafasi yake anastahili kuchangia  kwani ni aibu sana ikiwa baadhi ya wanafunzi 300 watapelekwa shule ya sekondari Benjamin Mkapa na Songambele huku 400 watakosa madawati," alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo wadau wa madini Mererani Dkt. Jacob Shegga mkurugenzi wa Covenant Ltd na Kilia Laizer wamesema kuwa suala kulipia huduma za jamii ni jambo ambalo hawalipingi na limekuja wakati muafaka ila utaratibu uboreshwe na uwe endelevu ili kuweza kuboresha kijiji chetu.

Walisema kuwa mkanganyiko wanaoupata umetokana na akaunti kuchanganywa na kuomba mji mdogo uwe na akaunti ya malipo ya huduma za jamii pekee ili kuwaondolea suala hilo la mkanganyiko huo.

No comments:

Post a Comment