NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKAGUA MAANDALIZI UJENZI WA BARABARA IENDAYO CHUO CHA VIONGOZI KIBAHA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 24 December 2019

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKAGUA MAANDALIZI UJENZI WA BARABARA IENDAYO CHUO CHA VIONGOZI KIBAHA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa (mwenye suti nyeusi) akipata maelezo toka kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere leo mjini Kibaha alipokagua ujenzi wa barabara iendayo katika chuo hicho cha viongozi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa (mwenye suti nyeusi) akikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara iendayo katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere leo mjini Kibaha. Barabara hiyo inayoanzia kibaha Kwamfipa hadi kilipo Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere mjini Kibaha inajengwa na wadau wa aina tatu ambao ni TANROADS Km 1.9, pamoja na TARURA Km 0.18.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa (katikati) akizungumza jambo akiwa katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere leo mjini Kibaha, alipofanya ziara kukagua ujenzi wa barabara iendayo katika Chuo hicho cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere mjini Kibaha.
Ujenzi wa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere ukiendelea. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Kwandikwa leo alikagua ujenzi wa Barabara inayoelekea katika chuo hicho inayoanzia Kibaha Kwamfipa inajengwa na wadau wa aina tatu ambao ni TANROADS Km 1.9, pamoja na TARURA Km 0.18.
Naibu Waziri Mh. Kwandikwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali toka ndani na nje ya nchi walipotembelea Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment