![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi. |
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwezekano wa kutokea kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinazoendelea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi pamoja na kanda ya kati zinatarajiwa kusambaa katika maeneo mengine ya nchi. Hali hii inatokana na kuimarika kwa ukanda mvua na kusogea zaidi katika
maeneo hayo.
Hivyo, tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa kwa siku ya kesho tarehe 21/12/2019 inatolewa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida, Lindi, Mtwara, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha, kwa tarehe 22/12/2019 vipindi hivyo vya mvua kubwa vinatarajiwa kupungua. Hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa Angalizo la mvua kubwa. Kutokana na uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa kaskazini mashariki mwa Madagascar TMA inaendelea kufuatilia mwenendo wa mgandamizo huo pamoja na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa nchini.
USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua. Imetolewa na;
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


No comments:
Post a Comment