WATANZANIA WATAKAOSHINDA KILIMANJARO MARATHON 2020 KUTIA KIBINDONI SH. MIL. 7 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 3 November 2019

WATANZANIA WATAKAOSHINDA KILIMANJARO MARATHON 2020 KUTIA KIBINDONI SH. MIL. 7



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifurahi mara baada ya  kufunua pazia kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020,  kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki. 

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia ni Woinde Shisael  Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. Mashindano hayo yatafanyika Machi Mosi mwakani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020,  kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia niWoinde Shisael  Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto), akikabidhiwa zawadi na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.



Meneja wa Grand Malt, David Tarimo wadhamini wa mbio za Km 5, akielezea kuhusu udhamini huo pamoja na sifa za kinywaji hicho.




Woinde Shisael  Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon akielezea kuhusu udhamini wao na kuwaomba watanzania kuisapoti kampuni hiyo kwa kujisajili kwa wingi kujiunga na mtandao huo mkubwa nchini.

No comments:

Post a Comment