ZIARA YA NAIBU WAZIRI KWANDIKWA KIGOMA NA TABORA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 2 October 2019

ZIARA YA NAIBU WAZIRI KWANDIKWA KIGOMA NA TABORA

Muonekano wa barabara ya Mwandiga-Chankere-Mwamugongo Km 45, ambayo ujenzi wa kuifungu ili ipitike umeanza, kukamilika kwa barabara hiyo inayounganisha Tanzania na Burundi kupitia tarafa ya Kagunga kutachochea huduma za utalii, kilimo na biashara mkoani Kigoma.

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma (wa pili kushoto), akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa (kushoto), alipokagua eneo litakalotumika kurefusha njia ya kuruka na kutua ndege katika uwanja wa ndege wa Kigoma, kulia ni meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Bw, Theophany Bileha.

Muonekano wa barabara ya Urambo-Kaliua Km 28, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Tabora.

Muonekano wa barabara ya Urambo-Kaliua Km 28, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Tabora.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akifafanua jambo kwa meneja mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua Km 28, Eng. Protas Mwasyoke alipokagua ujenzi wake. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


No comments:

Post a Comment