TCRA NA KAMPENI YA MNADA KWA MNADA SENGEREMA UTOAJI ELIMU YA USAJILI WA LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 18 October 2019

TCRA NA KAMPENI YA MNADA KWA MNADA SENGEREMA UTOAJI ELIMU YA USAJILI WA LAINI KWA ALAMA ZA VIDOLE


Wananchi wakipata huduma ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika Viwanja Nyahunge.

Mhandisi Francis Mihayo akizungumza na wananchi wakati wa Kampeni ya Mnada kwa Mnada uliofanyika katika Viwanja vya Nyehunge Sengerema.

Baadhi ya wananchi wakisoma vitabu vya muongozo wa TCRA katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Nyehunge Sengerema.

KAMPENI ya Mnada kwa Mnada iliyoanza Oktoba 11 katika maeneo ya Kome Pamoja Maisome kwa siku mbilimbili ikiwa ni kuwafikia wananchi wengi katika wilaya hiyo imeendelea kushika kasi.

Akizungumza katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada katika Viwanja vya Nyehunge Wilayani Sengerema Mkuu wa Kanda Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema wamejipanga kuwafikia wananchi wote wawemejisajili laini za simu kwa alama za vidole.

Mhandisi Mihayo amesema katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wapo katika kusajili wananchi vitambulisho kwa ajili ya kufanya Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Wakazi wa Nyehunge Wilayani Sengerema na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji  kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 16 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo katika kuwawezesha wananchi kupata elimu ya Mawasiliano Pamoja usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Amesema ni fursa kwa wananchi wa Sengerema kujitokeza kujisajili laini za simu kwa alama za vidole na  huduma nyinginezo  kutokana  na kuwepo kwa mnyororo   wadau wa  mawasiliano.

Aidha Mihayo  amesema kuwa  Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ili wasiweze kumuacha mtu yeyote kutotumia simu ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

Amesema muda uliopo ni miezi mitatu hivyo Wananchi wakamilishe taarifa zinazohitajika katika kujisajili laini za simu  kwa alama  za vidole ili kuondoa usumbufu mwisho wa Desemba kwa watu kupanga foleni.

Mhandisi Mihayo amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema  kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Mhandisi Mihayo amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

"TCRA tupo tayari  kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Mhandisi Mihayo.

Nae Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TCRA Mabel Masasi amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kwa Wananchi kutaka vitambulisho kwa ajili ya kusajili laini za simu kwa alama za vidole hali na kufanya wananchi wengi wamepata vitambulisho vya Taifa na kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Masasi amesema  Wananchi wa watumie Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA kupata elimu na baada ya kuisha Mnada sehemu husika waende katika mamlaka husika kupata vitambulisho.

Ameongeza kuwa watahakikisha kila mwananchi anajisajili kwa alama za vidole kwani Watu wana haki ya kuwa na mawasiliano ya simu.

No comments:

Post a Comment