Mwenyekiti
wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (katikati)
akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa TTCL kufurahiya
mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na ujumbe mfupi(SMS)
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi
Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba pamoja na Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi. Lulu Mkudde.
Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri (kulia) akipongeza moja ya kikundi cha burudani kwenye hafla ya uzinduzi huo. |
Mmoja wa wateja wa TTCL akipata huduma kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Bando la TamTam. |
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya T-PESA
imezinduwa huduma mpya ya Bando la TamTam ambalo linampa uhuru zaidi mteja wa
TTCL kufurahiya mawasiliano nafuu ya huduma ya maongezi, inatenti pamoja na
ujumbe mfupi (SMS).
Huduma hiyo
imezinguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya T-PESA, Brigedia
Generali mstaafu, Ramadhan Kimweri huku akisisitiza kuwa bidhaa hiyo imebuniwa
kwa lengo la kuendelea kurahisisha huduma kwa wananchi kwa bei nafuu zaidi.
Aidha aliwaomba Watanzania na wateja kwa ujumla kuendelea kutumia huduma za
T-PESA ikiwa ni pamoja na kufurahiya mawasiliano ya huduma mpya ya Bando la TamTam.
“...T-PESA
inawaletea huduma bora ya kipekee kabisa ya BANDO ambalo ni NAFUU na
lenye MVUTO wa aina yake kwa
watumiaji. Wananchi watapata fursa ya kupata huduma kwa siku, wiki na mwezi
ikiwa na muda wa maongezi, huduma ya Inatenti na ujumbe mfupi (SMS),” alisema
Bw. Kimweri.
Awali
akifafanua juu ya huduma ya Bando Tam Tam la T-PESA, Afisa Mkuu wa T-Pesa, Bi.
Lulu Mkudde alisema huduma hiyo itakuwa na virushi vya aina tatu, ambayo ni
pamoja Kifurushi cha Siku, ambacho kinampa
mteja MB 500 za kutumia intaneti, SMS 50 na dakika 5 za kupiga simu mitandao
yote kwa masaa 24 kwa shilingi 500 tu.
Alibainisha kuwa Kifurushi cha pili cha Wiki, ambacho kinampa mteja GB 1 ya kutumia intaneti, SMS 100
na dakika 5 za kupiga simu mitandao yote kwa siku 7 za wiki kwa shilingi 1000,
huku akikitaja Kifurushi cha tatu cha
Mwezi, ambacho kinampa mteja GB 2 za kutumia intaneti, SMS 300 na dakika 20
za kupiga simu mitandao yote kwa siku 30,kwa shilingi 5000 tu.
Aidha
alibainisha kuwa ili kuendelea kuboresha huduma za T-PESA, kampuni imeendelea
kusajili mawakala nchi nzima hadi kufikia sasa T-PESA inamawakala wanaozidi
zaidi ya 19,000 nchi nzima, uwepo wa mawakala hao wamechangia katika kufikisha
huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini.
“... T-PESA
imekuwa miongoni mwa kampuni zenye gharama nafuu za miamala kulinganisha na
watoa huduma wengine. Hivyo watanzania wanahaki ya kujivunia zaidi na kutuunga
mkono zaidi kwa kutumuia huduma zetu za T-PESA.” Alisisitiza.
“...Vifurushi
hivi vinapatikana kwa mteja wa T-PESA. Jinsi ya kujiunga ni rahisi, mteja
anatakiwa kupiga*150*71#. kuchagua
namba 3 kununua Muda wa Maongezi au Vifurushi, halafu namba 2 kununua
Vifurushi, kisha kuchagua namba 1 Bando Tam Tam.”
No comments:
Post a Comment