SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA KODI KIWANDA CHA KILIMANJARO FRESH - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday 20 October 2019

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA KODI KIWANDA CHA KILIMANJARO FRESH

Picha ikionyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania, Abdallah Ulega akikagua maziwa aina ya Kilimanjaro Freshi yanayotengenezwa na kiwanda cha KILIMANJARO Fresh wakati alipofanya ziara yakutembelea  kiwanda hicho jana kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha ambapo aliwasihi watanzania kupenda kutumia vyakwao na sio bidhaa za nje ya Nchi (picha na Ahmed Mahmoud, Arusha).

Na Ahmed Mahmoud Arusha

SERIKALI imeaidi kutatua changamoto kubwa inayokikabili kiwanda cha usindikaji wa maziwa cha Kilimanjaro fresh cha jijini Arusha kinachokabiliwa na changamoto ya ukubwa wa kodi ya ongozeko la thamani ambalo inabidi kushindwa kufikia uzalishaji mkubwa wa maziwa kama uhitaji wake ulivyo mkubwa kwa jamii.
Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Freshi jijini Arusha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ullega amesema kwamba serikali kupitia wizara yake itaakikisha inaondoa changamoto hiyo ya tozo kwa lengo la kuimarisha uzalishaji wa usindikaji wa maziwa katika kiwanda hicho cha Kilimanjaro fresh Milk.
Ullega amesema kwamba kiwanda hicho toka kuanzishwa kwake miesi 6 kimekua na mafanikio mkubwa   ili mpate mafanikio zaidi lazima mnunue kwa bei kubwa zaidi kutoka kwa wafugaji ambao watapata nguvu ya kuweza kuzalisha zaidi na kuongeza thamani ya uzalishaji wenye uboira unaohitajika.
Amesema kuwa mmesema kuwa mtatoa motisha ya mitanda endeleeni na zoezi hilo kwa kuwa ni sehemu ya kuongeza motisha kwa wafugaji kuongeza uzalishaji kwenye bidhaa za maziwa hapa nchi nanyi kuweza kuongeza uzalishaji wa maziwa kwenye kiwanda hicho na muendelee kufuata maagizo ya serikali kwa ajili ya kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo.
Alisema kuwa kiujumla wameeza vizuri katika uzalishaji wenye tija na nimependa utoaji wenu wa elimu kwa wafugaji kuwapa elimy ya ulishaji wa chakula vizuri mrudie agizo la waziri mkuu kwa kiwanda cha maziwa Asas kwenye wiki ya maziwa Kilimanjaro muandike barua wizarani  kuhusu malalamiko yenu nasi tutayafanyia kazi haraka kwa faida ya ukuaji wa tasnia.
Awali akitoa maelezo ya Kiwanda hicho  mkurugenzi wa kiwanda hicho cha Kilimanjaro Fresh  Irfhan Virjee alimweleza mh,Naibu waziri changamoto zinazo mkabili katika uzalishaji wa maziwa kua tozo ni changamoto ya kodi ya vat ambapo ameomba kuondolewa.
Alisema kuwa mwezi wa kwanza mwaka 2020 wanataraji kuzalisha lita zipatazo elfu 20 ambapo pia wanataraji kuanza kuuza maziwa nje ya nchi ambapo walianza kuzalisha kuzalisha  lita elfu 3000 hadi sasa wanazalisha lita 800kwa siku.
Alisema kwamba kiwanda hicho kimekuwa mkombozi kwa wafugaji  kutoka vyama vya ushirika ambapo huwauzia maziwa kwa kiasi cha shi;lingi 800 hadi kufikia shilingi 850 ambapo pia wakulima hupatiwa motisha kwa lengo la kuendelea kutunza mifugo kwa lengo la kuboresha mifugo kupata maziwa yalio na ubora wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment