Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akihamasisha
mafundi Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Vingunguti kwa kushiriki kazi hizo.
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa ukiendelea Vingunguti jijini Dar
es Salaam.
Ujenzi wa Machinjio ya kisasa ukiendelea Vingunguti jijini Dar
es Salaam.
TANGU Rais Dk. John Pombe Magufuli, alipotembelea ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti hivi karibuni na kuangiza ujenzi huo uwe umekamilika ndani ya miezi mitatu ijayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameendelea kusimamia ujenzi huo usiku na mchana.
Usimamizi huo unaonekana kuanzaa kuzaa matunda ya haraka
jambo ambalo sasa anadai kufurahishwa na kasi ya ujenzi huo kiasi cha kumpa
matumaini ya kukamilika ndani ya miezi mitatu iliyotolewa.
Akizungumzia ujenzi huo, Makonda amesema kuwa, katika jambo ambalo
Watanzania walifanya kwa isahihi na kwamba hawatakuja kujuta kufuatia maendeleo
yake, ni pamoja na kumchagua Rais Magufuli kuwa rais wa nchi hii.
Kwa maana hiyo uamuzi wa kufanya hivyo hakika wanatakiwa
kutambua kuwa walichagua maendeleo ya ujenzi wa miundombuni sahihi kama,
mabarabara,Hospitali,shule na sasa machinjio makubwa na ya kisasa kabisa ya
vingunguti.
Kwa maana hiyo anawaomba watanzania waendelee kuunga mkono
juhudi zake kwani yeye na viongozi wengine hawatachoka kumsaidia ili kufikia
malengo bora aliyokusuhudia kuwafanyia watanzania wote kipindi chote cha
uongozi wake.
No comments:
Post a Comment