Diwani wa kata ya Kihesa manispaa ya Iringa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake Kihesa
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
ZAIDI milioni mia mbili
zimetumika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu,miundombinu, afya na utamaduni
katika kata ya Mapanda iliyopo katika jimbo la Mufindi kaskazini ikiwa ni
kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.
Akizungumza na blog hii diwani
wa kata hiyo Jully Sawani alisemakuwa katika sekta ya elimu wamefanikiwa
kujenga majengo mapya katika shule mbalimbali zilizopo katika kata hiyo
kwaushirkiano wa serikali, wananchi na wadau mablimbali wa maendeleo waliopo
katika kata hiyo.
“Nguvu ya wananchi ilikuwa ni
mchanga na mawe tu, mfano shule ya sekondari ya kihesa ilikuwa inakabiliwa na
ukosefu wa majengo, viti, meza za walimu na miundombinu ya shule haikuwa rafiki
kabisa katika namna ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa shule na hivyo hivyo
katika shule za msingi ngome na Kihesa ambazo nazo zilikuwa zinakabiliwa na
tatizo la vyoo na uchakavu wa miundombinu lakini tumefanikiwa kutatua tatizo
hilo,” alisema Sawani
Sawani alisema kuwa katika
sekta ya afya amefanikisha zoezi la wazee na kupewa huduma bure, tatizo la
madawa nalo wamefanikiwa kulitatua na kufanikiwa kuboresha huduma bora kwa
kutoa elimu kwa wafanyakazi kutoa huduma bora kwa wagonjwa na wateja wote ambao
wamekuwa wanapata huduma katika kituo hicho.
“Saizi ukienda katika kituo cha
afya cha ngome unahudumiwa vizuri tofauti na ilivyokuwa hapo awali hiyo
kutokana na elimu ambayo walipata wahudumu wote wa kituo hicho kutoka kwa
wataalamu wa huduma makazini na ndio sababu ya sasa kutolewa huduma bora
kabisa,” alisema Sawani
Aidha Sawani alisema kuwa swala
la barabara limekuwa changamoto kubwa kutokana na barabara hizo kuharibika mara
kwa mara na zinatumia gharama kubwa kukarabati miundombinu hiyo lakini kuna
barabra ya kutoka ngome kwenye shule sekondari ya Kihesa, mwachang’a kwenda kanisani na majengo mapya.
“Ili kurahisisha maendeleo
lazima kuwe na miundombinu bora hivyo nimepigana navyoweza kwa ushirikiano
mkubwa na chama cha mapinduzi tumefanikiwa kutatua kero hiyo kwa kiasi chake,” alisema Sawani.
Sawani alisema kuwa tatizo la
maji linaelekea kutatuliwa kutokana najuhudi zinazofanywa kuhakikisha wananchi
wa kata hiyo wanapata maji kwa kutumia mamilioni ya fedha kutoka kwa wadau na
serekali ambapo wananchi wameshachanga na serikali tayari imeleta wataalamu kwa
ajili ya kutatua kero hiyo.
No comments:
Post a Comment