BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KM 107,4 KUKAMILIKA MWAKANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 1 August 2019

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KM 107,4 KUKAMILIKA MWAKANI

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Moronga- Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Muonekano wa box calvat linalojengwa katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe. 

Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Bw, Ali Kassinge akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua ujenzi wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Muonekano wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe. 

Mkandarasi China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG), akiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4

Mhandisi mshauri Adarsh Nayyar akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua mtambo wa kuchakata kokoto zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 mkoani Njombe.

Muonekano wa nyumba ya Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete zinazojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe.

Muonekano wa bweni la wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe. Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Julai 31,2019.

No comments:

Post a Comment