Wakazi wa kijiji cha Weru 1 Kata ya Wasa wakicheza ngoma ya asili na mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga mara baada ya kuwasili kwa ajili ya ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal).
Wakazi wa kijiji cha Weru 1 Kata ya Wasa wakisikiliza hotuba ya mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019.
Wakazi wa kijiji cha Iganduka Kata ya Wasa wakisikiliza hotuba ya mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kijimbo ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo tarehe 26 Julai 2019.
Na Mathias Canal, Songwe
MBUNGE wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mhr John
Palingo kumkamata mfanyabiashara aliyewauzia wakulima mbegu feki katika wilaya
hiyo hivyo kuathiri mavuno kwa wakulima.
Waziri Hasunga ameyasema hayo wakati wa mikutano
yake katika kijiji cha Isalalo, Wasa na Malolo vilivyopo katika kata ya Wasa
kadhalika akiwa katika kijiji cha Msia, Weru 1 na Iganduka vilivyopo katika kata ya Msia.
Waziri huyo wa Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa
kitendo cha mtu kuuza pembejeo feki ni cha uhujumu wa Kilimo na uchumi na
kwamba serikali haiwezi kuvumilia hali hiyo.
"Katika hili namwagiza mkuu wa wilaya
kumkamata msambazaji wa mbegu hizo ili hatua za kisheria ziweze
kuchukuliwa" alisema Hasunga.
Kauli hiyo ameitoa kufuatia swali la mkulima mmoja
mkazi wa Kijiji cha Malolo Ndg Isaya Nyondo ambaye alitaka kujua hatua zipi
zinachukuliwa na serikali kufuatia kuuziwa mbegu feki na hivyo kufanya
washindwe kuvuna mwaka huu.
Mhe Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli imekusudia kuimarisha sekta ya Kilimo hivyo mfanyabiashara yeyote
anayecheza na ufanisi wa wakulima atachukuliwa hatua Kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment