KWANDIKWA: TAASISI ZA SERIKALI SHIRIKIANENI MPATE TIJA KWA HARAKA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 31 July 2019

KWANDIKWA: TAASISI ZA SERIKALI SHIRIKIANENI MPATE TIJA KWA HARAKA


Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Njombe  - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akikata mfuko wa saruji aliposhiriki kazi ya kusambaza saruji katika ujenzi wa barabara ya Njombe  - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami.



Mhandisi Lusekelo Kijalo (kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Njombe - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami, kulia ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana.

Muonekano wa barabara ya Njombe  - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe.



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akitazama ubora wa lami inayojengwa katika barabara ya Njombe  - Moronga km 53.9.


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana (kulia) na Mhandisi Lusekelo Kijalo (kushoto), alipokagua ujenzi wa barabara ya Njombe  - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mheshimiwa Elius John Kwandikwa amezitaka Taasisi za Serikali mkoani Njombe kufanyakazi kwa kushirikiana na bidii ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora na za uhakika kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara na nyumba za Serikali mkoani humo Mhe. Kwandikwa amesema ni vema taasisi hizo zikawa na malengo yanayofanana katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
“Hakikisheni TANROADS,TARURA, TBA,TEMESA,TANESCO, Mamlaka za maji  na nyingine mnashirikiana kikamilifu ili huduma za miundombinu zinazojengwa kimkakati ziwe na tija za haraka kwa wananchi na kuwaletea maendeleo,”amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Naibu waziri huyo amesema barabara zikijengwa zinavutia ujenzi wa nyumba bora hivyo ni vema barabara zinapojengwa na miondombinu ya maji na umeme ikajengwa ili kurahisisha huduma za lazima kwa wananchi badala ya kusubiri mradi mmoja unapokamilika ndipo mradi mwingine uanze. 
Amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana kuhakikisha anamsimamia kikamilifu mkandarasi China Henan International Cooperation Group Company Limited (CHICO), anayejenga barabara ya Njombe - Moronga km 53.9 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe –Ndulamo-Makete km 107.4 ili atumie kipindi kisicho cha mvua kukamilisha barabara hiyo ili kuepuka visingizio pindi mvua zitakapoanza.
Aidha Naibu Waziri Kwandikwa amempongeza mkandarasi CHICO kwa kujenga madarasa mawili na bwalo katika shule ya msingi Ramadhani mjini Njombe ikiwa ni sehemu ya kusaidia ubora wa elimu nchini.
Amemwagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), mhandisi Abubakar Shahani  kuhakikisha majengo ya nyumba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe na Katibu tawala wa mkoa huo yanakamilika kabla ya Oktoba mwaka huu ili kuwawezesha viongozi hao kutumia nyumba hizo.
Naye meneja wa TBA mkoa wa Njombe mhandisi Shahani  amezungumzia changamoto za umeme na maji kuwa kikwazo katika kazi ya ujenzi wa ofisi mpya ya mkuu wa mkoa huo na kusisitiza kama suala hilo litapatiwa ufumbuzi miradi ya TBA mkoani Njombe itakamilika kwa wakati.
Naibu Waziri Kwandikwa yuko mkoani Njombe kwa ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya miundombinu katika sekta ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano. 
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Julai 30, 2019.


No comments:

Post a Comment