WASTAAFU 10,500 WA PSSSF BADO KUHAKIKI TAARIFA ZAO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 11 June 2019

WASTAAFU 10,500 WA PSSSF BADO KUHAKIKI TAARIFA ZAO

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Bw. Francis Nanai (kulia), akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) huku Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Bakari Machumu akishuhudia wakati wa ziara ya meneja huyo ikiwa ni muendelezo wa kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.

Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), wakiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN), chini ya Kaimu Mhariri Mtendaji, Bw. Januarius Maganga (wakwanza kulia), ikiwa ni muendelezo wa ziara ya meneja huyo kiongzi kutembeela vyombo vya habari kwa nia ya kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo mpya.

Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (kushoto) akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.

Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji mashuhuri wa luninga ya Azam TV, Charles Hillary na Ivona Kamuntu.

Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) na Bw. Abdul Njaidi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha XXL, cha Clouds FM, kutoka kushoto, B12, Kennedy the Remedy, na DJ.
Na Khalfan Said, Dar

JUMLA ya wastaafu 10,500 bado hawajafika kwenye ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuhakiki taarifa zao hadi sasa kwa mujibu wa utaratibu. Hayo yamesemwa na Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Eunice Chiume kwa nyakati tofauti wakati akitembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.

Alisema, zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu huwa linafanyika kila mwaka na huu ni utaratibu wa taasisi za hifadhi ya jamii na kwa upande wa PSSSF zoezi lilianza Desemba mwaka jana (2018).

Vyombo vya habari alivyotembelea leo Juni 11, 2019 kwa lengo la kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni mpya ni pamoja na magazeti ya serikali Tanzania Standard News Papers (TSN), Azam Media, wamiliki wa Azam TV na Uhai FM, Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Citizen na Mwanaspoti na Clouds Media Group, wamiliki wa Clouds TV na Clouds FM.

"Tangu Mfuko huu uanze shughuli zake Agosti 1, 2018 PSSSF ilifungua ofisi nchi nzima Bara na Visiwani na hivyo tunatoa wito kwa wastaafu wote ambao bado hawajahakiki taarifa zao kufanya hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima na wala hawalazimiki kuja makao makuu Dodoma kupatiwa huduma hiyo." Alifafanua Bi. Eunice Chiume.

Zoezi la kuhakiki taarifa hufanyika kila mwaka kwa upande wetu tulianza zoezi hili Desemba mwaka jana (2018) na liliendelea hadi Machi 2019 na tumeanza tena na zoezi hilo nab ado linaendelea.

“kuhakiki taarifa ni muhimu kwani kunasaidia kujiridhisha na taarifa za wastaafu wetu kwa sababu huwa kunakuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoaja na kujua kama bado wapo, au taarifa zao za kibenki zimebadilika au la na hii inasaidia kufanya malipo sahihi na kwa mtu sahihi.” Alibainisha.

Meneja huyo Kiongozi alitoa wito kwa wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa PSSSF iko imara katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wake wote popote pale nchini. “Mafao yenu yapo wastaafu wote, nendeni mkahakik taarifai, na hata ndugu ambao ndugu zao wastaafu ni wagonjwa wafike kwenye ofisi zetu na sisi tutakwenda kufanya uhakiki huko huko aliko.” Alifafanua Bi. Enice Chiume ambaye anaendelea na ziara yake Jumatano Juni 12, 2019.

No comments:

Post a Comment