WAFANYAKAZI WA BENKI YA DUNIA WAFANYA USAFI WA FUKWE JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 22 June 2019

WAFANYAKAZI WA BENKI YA DUNIA WAFANYA USAFI WA FUKWE JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird (kushoto) akiwa amejumuika na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo baada ya kuhitimisha zoezi lililofanyika katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Carlos Mdemu (wa tatu kushoto) ambaye ni Mratibu wa Nipe Fagio baada ya kuhitimisha zoezi hilo lililofanyika katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach wafanyakazi hao walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.Pichani walioinama chini ni vijana wa Nipe Fagio wakijaribu kufanya tathmini ni taka gani zaidi zimejitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la usafi katika fukwe hizo.

 Mratibu wa Nipe Fagio, Carlos Mdemu na vijana wake wakichambua sehemu ya taka za plastiki ziliookotwa na wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam huku Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia (WB) nchini, Bella Bird na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakitafuta ufumbuzi wa kuhakikisha bahari inakuwa safi na salama kwa viumbe wanaoishi baharini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiokota taka za plastiki zikiwemo chupa za vinywaji vya MO Energy vya kampuni ya MeTL na mifuko ya lambalamba za Ukwaju zinazotengenezwa na kampuni ya Azam iliyokuwa imetapakaa katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe  hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakionyesha taka za plastiki ikiwemo miraji na mifuko ya lambalamba bidhaa za Ukwaju zinazotengenezwa na kampuni ya Azam iliyokuwa imetapakaa katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe  hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiwa wamebeba mifuko ya kuhifadhi taka walipokuwa katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe  hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Ofisa Habari wa Benki ya Dunia nchini, Loy Nabeta akionyesha mifuko plastiki ya lambalamba za kampuni ya Azam iliyokuwa imezagaa katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe  hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakirejea na mifuko iliyosheheni taka za plasitiki baada ya kuhitimisha zoezi hilo eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi  wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mifuko ya kuhifadhia taka baada ya kuhitimisha zoezi lililofanyika katika eneo la fukwe za bahari ya Coco Beach walipojitolea kusafisha fukwe hiyo ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

Baadi ya taka za mifuko plastiki ya lambalamba za kampuni ya Azam pamoja na chupa za vinywaji vya kampuni ya MeTL zilizochambuliwa na vijana wa Nipe Fagio baada ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya  Tanzania kumaliza zoezi la usafi katika fukwe za bahari ya Coco Beach ikiwa ni juhudi za kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira jijini Dar es Salaam.

WAFANYAKAZI wa  Benki ya Dunia ofisi Tanzania  wakiongozwa na Mkurugenzi wao, Bi. Bella Bird, wamefanya  usafi kwenye fukwe za bahari eneo la Coco Beach jijini Dar Es Salaam. 
Usafi huo ulifanyika kama jitahidi za Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania kuunga mkono mpango wa serikali kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ilikua ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa mazingira.

“Ujumbe wetu kwa jamii ni wawe na wajibu wa kuepuka uchafuzi,  kuondoa utamaduni wa kutupa taka ovyo na kua na tabia ya kuchakata. Tumefurahi Serikali imechukua hatua kubwa kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki na tunatumaini wataendelea kudhibiti",alisema Bi.Bird.
Aliendelea kusema kwamba upungauaji wa taka za mifuko ya plastiki hakika ni kitu kikubwa kwa Tanzania kusherehekea. Pia alisema hatua itayofuata ni kupiga marufuku mirija ya vinywaji kwa kua haina matumizi yoyote muhimu kwa karne hii.

Nao wafanyakazi wa Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania walisema kila mmoja ana jukumu la kutunza mazingira.
"Wote tunajukumu kwenye  hizi taka. Makampuni ya vyakula na vinywaji  yashiriki kutoa elimu kwa jamii, kupanga usafi, kuweka pipa za taka na kusaidia uzoaji taka kama jukumu la kampuni kwa jamii",walisema wafanyakazi hao.

Nae, Carlos Mdemu ambaye ni mratibu wa  'Nipe Fagio' alisema “kuweka pipa za taka maeneo ya fukwe na mtaani ni mpango mzuri, lakini kwenye baadhi ya maeneo tumeona mapipa yanajaa na hakuna  anayekuja kuyazoa, kwahiyo watu wanabidi wajue majukumu yao pia”.
 Mdemu aliendelea kusema “kuwatoza faini  kwa kutupa taka ovyo inafanywa na Manispaa ya Ilala na ni nzuri. Lakini kuongeza ufahamu inaweza kua muhimu zaidi ili kwamba watu wengi wakiwa wanajua, unapunguza nguvu ya kuwatoza faini”.

Kuhusiana na taka za plastiki Mdeme alisema “kwa sasa, taka yenye changamoto tuliyoona ni chupa za plastiki zenye rangi na vifungashio vya chakula (aiskrimu n.k).  Chupa za plastiki za rangi hazikusanywi kwa ajili ya kuchakata kwasababu hazina soko kwa  wakusanyaji”.
“Hapo nyuma tulipofanya usafi wa fukwe, tuligundua hesabu za taka za mifuko ya plastiki ni zaidi ya asilimia 50. Hii imebadilika, leo tumekusanya si zaidi ya asilimia 10” alisema Carlos Mdemu.  

 Wakihitimisha usafi katika fukwe za Coco Beach wafanyakazi hao walisema "tumeacha alama ndogo ukilinganisha na kinachotakiwa kufanywa. Lakini hii ndiyo sababu kwanini tumefanya na kwanini wote inabidi tuunganishe mikono na kuacha alama kubwa zaidi.
"Tunatekeleza tunachokisema, Benki ya Dunia Tanzania tunasema hapana kwa plastiki, weka fukwe na bahari yetu safi, sema hapana kwa matumizi ya plastiki, saidia mapambano dhidi uchafuzi wa plastiki" walisema wafanyakazi hao.

No comments:

Post a Comment