MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya kikao cha wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TMA kwa kujumuisha wafanyakazi kutoka Makao Makuu na Ofisi ya Kituo Kikuu cha Utabiri (CFO).
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kikao hicho, aliwataka wafanyakazi kujitathimini mapungufu yaliyopo ili kuboresha utendaji wa kazi za Mamlaka.
‘Ili kuboresha huduma zetu kama Mamlaka na kukidhi matakwa ya sheria mpya ya huduma za hali ya hewa nchini, tunatakiwa tujitahimini wenyewe mapugufu yetu ili tuweze kuboresha utendaji kazi wetu’. Alizungumza Dkt. Kijazi.
Aliendelea kwa kusisitiza bidii na weledi mahali pa kazi ili kuongeza ufanisi wa kazi za Mamlaka na kutambua kuwa jukumu letu ni kuhudumia wananchi wanaoitegemea TMA katika utoaji wa huduma za hali ya hewa. Aidha Dkt. Kijazi aliwakumbusha wafanyakazi kuhusiana na kuvaa mavazi sahihi kulingana na taratibu za ofisi za umma pamoja na wale wanaohitaji huduma kutoka nje ya Mamlaka.
Dkt. Kijazi alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wafanyakazi wote kwa ushirikiano na upendo waliouonesha katika mchakato mzima wa uchaguzi wa kuwania nafasi ya umakamu wa tatu wa Rais wa WMO na mapokezi ya heshima kwake.
Menejiment ya TMA imeweka utaratibu wa kukutana na wafanyakazi wa Mamlaka ili kujadilia masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma zake sambamba na kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza katika kipindi husika. Mwenyekiti wa vikao hivyo ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA.
IMETOLEWA NA
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)
No comments:
Post a Comment