RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA, AIRTEL WATOA BILIONI 3 KAMA FIDIA NA DOLA MILIONI MOJA MCHANGO BINAFSI WA MWENYEKITI WA AIRTEL - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 10 June 2019

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA, AIRTEL WATOA BILIONI 3 KAMA FIDIA NA DOLA MILIONI MOJA MCHANGO BINAFSI WA MWENYEKITI WA AIRTEL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha, Bw. Charles Kichere kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es salaam Juni 10, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha, Bw. Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam Juni 10, 2019.
  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli pamoja na waalikwa akishuhudia Jaji mstaafu, Harold Nsekela ambaye ni Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Utumishi wa Umma akiwalisha kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bw. Charles Kichere na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Mhede Ikulu jijini Dar es salaam Juni 10, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya dola milioni moja za Kimarekani toka kwa Mwenyekiti wa Bharti Airtel, Bw. Sunnil Mittal ukiwa kama mchango wake binafsi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru, Ihumwa, Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Juni 10, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishuhudia Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi wa Shilingi Bilioni 3 zikiwa ni Fidia kwa serikali ya miezi mitatu kwa hesabu ya shilingi bilioni moja kwa kila mwezi ya Kampuni ya Airtel kwa  Serikali  toka kwa Mwenyekiti wa Bharti Airtel Bw. Sunnil Mittal kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Juni 10, 2019.

No comments:

Post a Comment