MATUKIO BUNGE LIKIPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI YA SH. TRILIONI 33.1...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 27 June 2019

MATUKIO BUNGE LIKIPITISHA BAJETI KUU YA SERIKALI YA SH. TRILIONI 33.1...!

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akifanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa na Bunge, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja za Wabunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa kwa kishindo Bungeni Jijini Dodoma.

Baadhi ya Mawaziri na  Wabunge wakifurahia baada ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kuidhinishwa na Bunge Jijini Dodoma. (Picha na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mawaziri wakati wakijibu hoja mbalimbali za Wabunge kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashugwa akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Bunge wakati wa majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20 kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kushoto), akiwa na Wakuu wa Idara na Taasisi za Wizara hiyo wakifuatilia majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kufanya majumuisho ya mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kabla ya kupitishwa Bungeni Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Sh. trilioni 33.1, katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. (Picha na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma.

No comments:

Post a Comment