MVUA ZAFUNGA BARABARA DAR, FOLENI ZA MAGARI ZAKERA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 13 May 2019

MVUA ZAFUNGA BARABARA DAR, FOLENI ZA MAGARI ZAKERA...!

SEHEMU ya barabara ya Kawawa eneo la bonde la Morroco kutokea Magomeni kuelekea vituo vya Mkwajuni, Studio na Manyanya likiwa limejaa maji kutokana na mvua zinazonyesha mfululizo jijini Dar es Salaam. Kutokana na maji hayo magari yalishindwa kupita hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Kutokana na mvua hizo mabasi ya mwendo kasi yanayofanya safari jijini Dar es Salaam yalilazimika kusitisha safari zake zinazopita Jangwani na Morocco baada ya barabara hizo kujaa maji. Kufungwa kwa barabara hizo kutokana na kujaa maji kulileta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hizo kuingia katikati ya jiji na wale wa kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Barabara zilizosalia zilikuwa na msongamano mkubwa wa magari jambo ambalo lilikuwa kero kubwa kwa watumiaji.

Sehemu ya barabara ya Kawawa eneo la bonde la Morroco kutokea Magomeni kuelekea vituo vya Mkwajuni, Studio na Manyanya likiwa limejaa maji kutokana na mvua zinazonyesha mfululizo jijini Dar es Salaam. Pichani gari la Mwendo kasi likijitahidi kuvusha abiria ili kwenda upande wa pili wa vituo vya Mkwajuni na Studio baada ya kushindwa kupita.

SEHEMU ya barabara ya Kawawa eneo la bonde la Morroco kutokea Magomeni kuelekea vituo vya Mkwajuni, Studio na Manyanya likiwa limejaa maji kutokana na mvua zinazonyesha mfululizo jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya askari wakiwa wamepiga kambi eneo hilo lililojaa maji ili kuzuia magari na watu kwa usalama wao.

Sehemu ya kipande cha barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ukitokea Magomeni likiwa limejaa maji na magari kushindwa kupita katika kipande hicho. Baadhi ya abiria walilazimika kuvuka kwa miguu huku maji yakiwa yamejaa usawa wa mapajani kwa mtu mzima. 

Wanafunzi wakiwa eneo la Jangwani barabara ya Morogoro kutokea Magomeni wakiwa wameshindwa kupita sehemu hiyo baada ya kujaa maji.

Baadhi ya wananchi wakitafakari namna ya kuvuka eneo hilo la Jangwani baada ya kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya wananchi wakitafakari namna ya kuvuka eneo hilo la Jangwani baada ya kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment