Moja ya Kifaa cha
kampuni inayojenga Reli ya Kisasa, SGR ya Yapi Merkez kikiunganisha reli hiyo katika
moja ya ziara ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makataibu
tawala takribani 400, Mei 14, 2019.
Na
Paschal Dotto-MAELEZO
NI Takribani Miaka
120 ambapo historia iliandikwa, mwaka 1912, Serikali ya Kikoloni nchini iliamua
kuimarisha sekta ya usafirishaji Kwa kujenga Reli, ambapo njia zake
ziliunganisha Miji hasa maeneo ya kilimo, uzalishaji na kibiashara, reli kuu
kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, hatimaye Kigoma na Tanga.
Ni dhahiri sasa
tunaona Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akifanya mageuzi makubwa Kwa
kujenga reli ya kisasa, maarufu SGR (Standard Gauge Railway) ambapo kwa
vyovyote tutasogeza nyuma zaidi kuhusu historia ya reli nchini, kwani Rais anatakeleza
Ujenzi wa Reli ya Kisasa, Standard Gauge Railway (SGR) kwa maslahi makubwa
kiuchumi.
Katika hafla ya uwekaji
wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya SGR awamu ya pili, Morogoro-Makutupola,
iliyofanyika 14, Machi, 2018, Rais Magufuli aliwakumbusha Watanzania kuwa
Tanzania imekuwa nchi ya pekee Barani Afrika katika kutekeleza mradi huo mkubwa
kwa pesa za walipa kodi wake.
“Kwa bahati nzuri,
hivi karibuni tulitembelewa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na
alishuhudia kwamba Tanzania tumetayarisha fedha zetu wenyewe, kwa nguvu zetu
wenyewe, na walipa kodi ni watanzania wenyewe, Tsh Trilioni 2.8 na kutangaza tenda
zilizokuwa wazi, makampuni zaidi ya 40 yalijitokeza kuwania tenda, na bahati
nzuri kampuni kutoka Uturuki ikashinda tenda hii,” alisema Rais Magufuli na
kuongeza kuwa Uturuki itatupa mkopo wa masharti nafuu kwa awamu zingine za
ujenzi, Rais akaongeza, “ kwa hiyo Tanzania tunaweza,"
Rais Magufuli
aliwataka watanzania kutambua fursa za upitapo mradi wa SGR na kuwataka wafanyabiashara
wakubwa, wadogowadogo, mama ntilie, kunufaika wakati wa ujenzi na mara baada ya
ujenzi, na kwamba itakuwa nguzo kubwa kwa usafarishaji kwenye maeneo hayo na
nchi nzima.
“Katika uchumi wa
nchi yoyote duniani, Sekta ya Usafirishaji ni muhimu sana, kwa hiyo Serikali
kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa kujenga reli ya
kisasa, SGR, ni moja ya Mwarobaini wa kutatua changamoto ya usafirishaji mizigo
na kulinda usalama wa barabara”. Alisikika mmoja wa wahandisi akiwaeleza
waliowatembelea.
Mageuzi ya Rais
Magufuli yanalenga kuwaimarisha wananchi, si tu wafanyabiashara bali hata
wasafiri kwa utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR yenye kasi ya
160km/saa utakuwa na faida kuwabwa kwani masaa 2.5 Dar es Salaam-Morogoro na
masaa tisa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ni dhahiri kutakuwa na Furaha
kubwa kwa watu kuwahi kufika Mwanza mapema badala ya saa saba usiku au kulala
Shinyanga.
“Ujenzi wa Reli hii
(SGR), kwa Tanzania siyo chaguo bali ni lazima, kwani hatua hii ilitakiwa
ifikiwe zamani, lakini sasa Rais Magufuli ameamua kutufikisha kwenye teknolojia
mpya katika sekta ya usafirishaji, kwani matatizo mengi ya barabara yanatokea
kwababu ya mizigo mizito, hakuna reli imara ya kubeba mizigo hiyo, kwa hiyo
ujenzi wa Reli hii ni maamuzi sahihi kwa Serikali yetu.”, Anaeleza Mkurugenzi
TRC, Masanja Kadogosa.
Kadogosa anasema,
Reli hiyo ambayo inatumia nishati ya umeme imekuja wakati mwafaka ikiwa
Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Mto Rufiji (Rufiji
Hydroelectric Power), wenye kutoa Megawati 2,115, kwa hiyo treni hiyo itapata
umeme wa kutosha.
“SGR, Ni mradi mkubwa
ambao unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufulu kwa
kutumia fedha za walipa kodi wake kwahiyo ni vyema watu wakafahamu kuwa kodi
yao inaenda wapi Trilioni 7 siyo mchezo”, alisema Kadogosa.
Ili kutekeleza adhima
ya kuutangaza mradi huo kwa wananchi, Mei 17, 2019, Jopo la Wakuu wa Mikoa,
Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Makatibu Tawala takribani
400 wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jafo
walitembelea kuona mradi huo ili kupeleka ujumbe kwa wananchi.
Kabla ya Safari hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa aliwapitisha kidogo wageni wake katika
shule ndogo kuhusu mradi ili kutambua umuhimu wa Mradi huo kwenye sekta ya
usafirishaji na kwa wananchi.
Masanja alieleza kuwa
Reli hiyo inayojengwa inaenda kufuta zana mbalimbaliikiwemo ile historia ya
kikoloni, kuwa reli iliyopo ilijengwa na wakoloni, lakini pia ujenzi wa Reli
hiyo sasa unaenda kuimarisha sekta ya usafirishaji. Serikali inatekeleza
ujenzi huo Kwa Kipande cha Dar es Salaam-Morogoro, Morogoro-Makutupola na badae
kutekeleza ujenzi huo hadi Mwanza, kilometa 1,219.
Kadogosa alisema kuwa
Reli hiyo, SGR inauwezo wa kubeba tani milioni, 10,000, kwa mkupuo sawa na
malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani 10,000 na kuwa na kasi kubwa ya
160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo inakasi ya 30km/saa, kwa Afrika itakuwa ni
Reli pekee yenye uwezo mkubwa kama huo, tani Miliomi 10-17 zitasafirishwa kwa
mwaka, kwa hiyo SGR ni mwamba sekta ya usafirishaji nchini.
Aidha, Kadogosa
alieleza kuwa ujenzi wa Reli (SGR), Dar es Salaam-Morogoro unatekelezwa na
Kampuni kutoka Uturuki, Yapi Merkezi takribani Trilioni 2.7, lakini kwa sehemu
nyingine ni Yapi Merkezi na Portuguese Construction Group Motel-Engil.
kukamilika kwa mradi
huo kutakuwa na ufanisi mkubwa kwenye sekta ya usafirishaji nchini kwa kubeba
mizigo tani nyingi lakini pia kasi yake katika kusafirisha abiria, kutoka Dar
es Salaam- Dodoma treni itakuwa inafanya safari mara nane kwa siku, kwa hiyo ni
hatua kubwa kwa sekta ya usafirishaji.
Kadogosa alizitaja
baadhi ya Faida za Mradi huo Kwa sasa kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla
kwani kwa sasa watanzania walioko sehemu za ujenzi wanafaidika na kupeleka
malighafi za ujenzi, mama ntilie kupika chakula na biashara zingine.
“Takribani mifuko ya
simenti milioni, 9,200,000 ambayo ni sawa na tani 600, nondo kilo milioni 115
sawa na tani 1500 na mataluma 1,400,000, kutoka kwa wasambazaji wa malighafi
hizo takribani 500, wafanyakazi 10, 000, huku asilimia 94 ya wafanyakzi hao ni
watanzania, pia asilimia 48 ya wataalam ni watanzania, kwa hiyo pamoja na mradi
huu kuwa nguzo imara ya usafirishaji
nchini, SGR imekuja kutoa Fursa za ajira kwa watanzania”, Alisema Kadogosa.
Kadogosa alisema kuwa
mradi huo ni mkubwa na uwezo wake ni wa juu, na sasa matatizo ya usafarishaji
nchini yatapata suluhu kubwa, kuimarisha na kulinda barabara nchini.
Katika sekta ya
usafirishaji wa mizigo hasa ile mikubwa inayotoka bandarini kwenda sehemu
zingine za nchi na mengine nje ya nchi, kwani kuwepo kwa Reli imara
itasababisha utendaji kazi wa bandari kuwa na ufanisi mkubwa, “Bandari inategemea
kuwepo kwa miundombinu imara kwa upande wa nchi kavu, hakuna ufanisi wa Bandari
bila kuwa na Reli imara, Serikali imeliona hilo ndiyo maana ikaamua kutekeleza
haraka ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Reli yetu hii inabeba mizigo mingi
Takribani Tani Milioni 17 kwa mwaka, hakuna Reli kama hii Barani Afrika,”
Kadogosa.
No comments:
Post a Comment