Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) Merry Lusimbi pamoja na washiriki wengine wakiwa katika hafla hiyo. |
Baadhi ya washiriki na meza kuu katika uzinduzi wa miradi mitatu mikubwa iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kupitia shughuli zao anuai unaofadhiliwa na Ubalozi wa Canada. |
Sehemu ya washiriki wakiwa katika hafla hiyo. |
Sehemu ya washiriki wakiwa katika hafla hiyo. |
Na Joachim Mushi
CANADA imejitolea kuunga
mkono juhudi zinazofanywa na Tanzania kusaidia uwezeshaji wanawake ili waweze kuzifikia
fursa na hatimaye kuchangia katika kujenga jamii bora yenye utamaduni wa kunufaika
kupitia ujasiriamali. Juhudi hizo zimeoneshwa baada ya kuzinduwa miradi mitatu
mikubwa iliyolenga kuwajengea uwezo wanawake kupitia shughuli zao anuai.
Akizungumza katika
uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Balozi wa Canada nchini
Tanzania, Pamella O’Donnell amesema mradi wa kwanza ambao wameuzinduwa
utaratibiwa na taasisi ya Shule Direct unaolenga kuwawezesha Wanawake
Wajasiriamali wabunifu kuanza biashara ili kumuendeleza yeye pamoja na jamii.
Miradi mingine miwili
itakayotekelezwa na TGNP Mtandao pamoja na Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF)
italenga kupaza sauti za wanawake na kuwawezesha kwenye uongozi ili waweze
kupigania haki zao na usawa wa kijinsia nchini Tanzania.
Balozi huyo, alisema ubalozi
wake unajivunia kufadhili miradi hiyo mitatu ambayo inalenga kupaza sauti za
wanawake na mradi wa uongozi utakaochochea uwezo wa wanawake kupigania haki na
usawa wa jinsia.
Uzinduzi wa miradi
hiyo umeenda sambamba na mjadala wa wazi uliojadili mada iliyosema Tanzania ya
Viwanda; mamlaka zinapaswa kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika
mchakato wa Tanzania ya viwanda.
Mjadala huo
ulioongozwa na Balozi, O’Donnell na kuwashirikisha Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP,
Bi. Lilian Liundi, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania na
Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Mkurugenzi wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) Merry
Lusimbi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Hope Centre for Children, Girls & Women
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shule Direct, Faraja Nyalandu
.
.
No comments:
Post a Comment