SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI, WADAU WA TMA WAIFAGILIA...! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 23 March 2019

SIKU YA HALI YA HEWA DUNIANI, WADAU WA TMA WAIFAGILIA...!


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (kushoto) akihutubia wadau wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Eng. Japhet Loisimaye akielezea namna taarifa zinazotolewa na TMA zinavyowasaidia wadau wa mamlaka hiyo kutekeleza majukumu yao, kwenye  hafla ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na TMA jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Elias Mwashiuya (kulia).

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari (katikati) akielezea jinsi taarifa zinazotolewa na TMA zinavyowasaidia wadau wa usafiri wa anga kutekeleza majukumu yao, kwenye  hafla ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na TMA jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Eng. Japhet Loisimaye (kulia).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Elias Mwashiuya akielezea namna wanavyonufaika na utabiri wa TMA kwenye hafla ya maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Eng. Japhet Loisimaye wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) akizungumza na wadau wa TMA katika maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Kulia ni wadau wa TMA wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhani Nyenzi (kushoto) akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (katikati) mara baada ya kuwahutubia wadau wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Dk. Kijazi akifuatilia.
 Wafanyakazi wa TMA wakiigiza igizo kuonesha umuhimu wa taarifa za utabiri kwenye maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Maadhimisho hayo yakiendelea.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe (katikati) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka za Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kulia) mara baada ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TMA, Dk. Buruhani Nyenzi akifuatilia.

Wadau wa TMA wakifuatilia igizo kwenye maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

No comments:

Post a Comment