|
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino (wa pili kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka 150, vitanda vya kulalia wagonjwa 11 pamoja na magodoro yake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Phillis Nyimbi kwa ajili ya Hospitali ya Butimba kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza. |
|
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino (wa pili kushoto) akimkabidhi msaada wa mashuka 150, vitanda vya kulalia wagonjwa 11 pamoja na magodoro yake Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Phillis Nyimbi kwa ajili ya Hospitali ya Butimba kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza. |
|
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk. Phillis Nyimbi (kulia) akizungumza kwenye Hospitali ya Butimba jijini Mwanza, wakati akipokea msaada wa mashuka 150, vitanda vya kulalia wagonjwa 11 pamoja na magodoro yake, msaada uliotolewa na Benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino. |
|
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Abraham Augustino (kushoto) akizungumza kwenye Hospitali ya Butimba wakati wa kutoa msaada wa mashuka 150, vitanda vya wagonjwa 11 na magodoro yake, kwenye hafla iliyofanyika Jijini Mwanza, kulia ni Mkuu wa Wilaua ya Nyamagana, Dk Phillis Nyimbi. |
KUTOKANA na maboresho yanayofanywa na Serikali katika miundo mbinu ya afya ikiwemo upatikanaji wa dawa, ujenzi wa zahanati, vituo vya afya na hosipitali, wadau wa maendeleo mkoani Mwanza wameendelea kuunga mkono jitihada hizo.
Benki ya NMB jijini Mwanza imetoa vitanda 11 na magodoro yake pamoja na mashuka 150 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuhudumia wagojwa katika Hosipitali ya Wilaya ya Nyamagana, Butimba mkoani Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. PHILIS NYIMBI na Meneja wa Benki ya NMB kanda ya ziwa ABRAHAM AUGUSTINO wanakiri Serikali kutambua umuhimu wa afya katika kuleta maendeleo.
Benki ya NMB imetoa msaada huo wa vitanda, magodoro na mashuka ikiwa ni sehemu ya shilingi bilioni moja iliyotengwa na benki hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja kuiunga mkono Serikali katika miradi ya kijamii.
No comments:
Post a Comment