NGOMA AFRICA BAND NA CD MPYA 'AWAMU YA TANO UWANJANI' - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 27 March 2019

NGOMA AFRICA BAND NA CD MPYA 'AWAMU YA TANO UWANJANI'

CD ya 'Awamu ya Tano Uwanjani'

SI wengine ni ile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni,inayoongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wenye makao yao nchini Ujerumani. Bendi hiyo imejizolea umaarufu kila kona barani ulaya na kufanikiwa kuteka washabiki kwa kutumia muziki wao wa dansi wa bongo.

Ngoma Africa band ukipenda waite FFU ughaibuni au viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" au "Watoto wa Mbwa" mara hii wamepakua CD yao "Awamu Ya Tano Uwanjani" yenye nyimbo mbili za "Amkeni Kumekucha"  na "Awamu ya Tano Sasa Kazi".

Nyimbo hizo ni utunzi na uimbaji wake Kamanda Ras Makunja akimshirikisha Chris-B  Bakotesa aka "Afande" ambaye pia ni  mpiga solo gitaa na kundi zima la FFU wa Ngoma Africa band wakisindikiza kwa mdundo mzima wa Hapa Kazi Kumpigia Saluti na  kumuunga mkono Rais Magufuli ,CD hiyo mpya imeshafika katika baadhi ya vituo vua redio hapa nchini.

No comments:

Post a Comment