Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Juma Mapesa
Makalah akimkabidhi fedha mmoja ya makepteini wa timu ambazo zilishiriki mashindano ya Lukuvi Cup ukanda wa Pawaga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ismani, Thom Malenga akiwa sambamba na diwani moja wa ukanda wa Pawaga wakati wa kuwazawadia washindi.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Isman William
Lukuvi amegawa zawadi za zaidi ya shilingi milioni arobain na moja kwenye
mashindano ya William Lukuvi cup yaliyofanyika katika kata zote kumi na tatu
katika jimbo hilo na kufanikiwa kuinua vipaji na kujenga afya kwa vijana
walioshiriki mashindano hao.
Akizungumza wakati wa ugawaji
wa vifaa hivyo katibu wa mbunge huyo Thom Malenga alisema kuwa wametumia zaidi
ya shilingi milioni arobain na moja kwa ajili ya kununua vifaa pamoja na kutoa
zawadi kwa washindi wa mashindano hayo kwa kila kata.
“Tumenunua mipira themenini (80)
kila mpira shilingi elfu thelathini (30,000) na jezi tumenunua themenini (80)
kila seti ya jezi inauzwa shilingi laki mbili na nusu (250,000) hapo kwa upande
wa vifaa tu vya michezo ambavyo tuligawa kila kijiji ambacho kipo jimboni kwetu”
alisema Malenga
Malenga aliongeza kuwa
mashindano hayo yalikuwa yanafanyika kwa kila kata hivyo mshindi wa kwanza
alijinyakulia kiasi cha shilingi laki saba (700,000), mshindi wa pili
alijinyakulia kiasi cha shilingi laki tano (500,000) na mshindi wa tatu
alijinyakulia kitita cha shilingi laki mbili na nusu (250,000),zawadi hizo
zilitolewa kwa kila kata ya jimbo hilo.
“Utaona tumetumia zaidi ya
shilingi million arobain na moja (41,250,000) kwa ajili ya vifaa na zawadi
katika mashindano haya ya Lukuvi cup kwa mwaka huu tu na kila mwaka tumekuwa
tukifanya mashindano haya kwa wananchi wetu wa jimbo letu la ismani” alisema
Malenga
Aidha Malenga alisema kuwa
mbunge wa jimbo hilo amekuwa na jitihada za makusudi za kusaidia timu za jimbo
hilo kwenye mashindano mbalimbali kwa lengo la kukuza michezo kwa wapenda
michezo wa jimbo hilo.
“Mimi naowaomba wanamichezo
kinapofika kipindi cha mashindano hayo wajitokeze na kuonyesha vipaji vyao na
kuweka sawa afya zao kwa kuwa sasa michezo ni ajira n analipa kweli kweli kama
ukiangalia mpira wa miguuu sasa ndia ajira ambayo inaongoza kwa malipo kwa
wachezaji hapa nchini” alisema Malenga
Kwa upande wake mwenyekiti wa
vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa Vijijini Juma Mapesa
Makalah alimpongeza mbunge wa jimbo hilo
kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo na kuinua na kuibua vipaji vya
wachezaji kutoka jimbo hilo.
“Kwa dhati kabisa nampongeza
mbunge huyu wa jimbo hili William Lukuvi kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta
maendeleo kwenye jimbo hili na kuinua michezo ni tofautia kwenye majimbo
mengine ya wilaya hiyo ambako hawajawahi kuona hata michezo ikianzishwa na
mbunge” alisema Makalah
Makalah aliongeza kwa kusema
kuwa wanamichezo wa jimbo la Isman wanabahati kuwa ya kuwa na mbunge anayependa
michezo huku akisema kuna jimbo la jirani tu wao kama viongozi hawajawahi hata
kusikia mbunge wa jimbo hilo ajishughulisha kwenye michezo.
“Jamani vijana wenzangu
waliulize majirani wezenu kama wamewahi kushiliki mashindano ya mbunge
waulizeni msiogope lakini nyie wa jimbo hili la Lukuvi mnacheza mashindano haya
kila mwaka na ndio faida ya kuwa na mbunge anayethamini vipaji vyenu” alisema Makalah
Lakini Makalah aliwaomba
wananchi wa jimbo la Isman kuendelea kuwanga mkono chama cha mapinduzi kwa
jithada ambazo zinafanywa na viongozi wao katika maeneo mbali mbali hapa nchi
kwa lengo kuleta maendeleo na kuwa wazalendo na nchi yao.
“CCM bado inawapenda na
itaendelea kuwapenda na kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo ya kila siku hivyo
naomba kwa niaba ya viongozi wangu kuendelea kuichagua CCM kwenye chaguzi zote
zinazokuja kwa ngazi zote na mtupe kula zote jamani ninaomba” alisema Makalah
No comments:
Post a Comment