GERMAN-AFRICA EXPO NA INTERN AFRIKA FESTIVAL TÜBINGEN 2019 UJERUMANI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 8 March 2019

GERMAN-AFRICA EXPO NA INTERN AFRIKA FESTIVAL TÜBINGEN 2019 UJERUMANI

WATAYARISHAJI wa maonesho makubwa ya German-Africa International Expo yanayokwenda sambamba na Afrika International Festival Tübingen, yatakayofanyika kuanzia 29 Julai mpaka 2 Augosti 2019 katika mjiwa Tübingen,nchini Ujerumani.

Wamefungua milango ya maombi kwa wale wanaotaka kushiriki katika maonyesho hayo, ambapo kutakuwa na maonesho ya makampuni ya kiafrika na bidhaa zao, maonyesho ya sanaa na utamaduni, na wale wenye makapuni ya shughuli za utalii wote mnakaribishwa kuwahi fursa.

Pia kutakuwa na semina ya wanahabari ambayo hiyo itakuwa ni maalumu kwa wanahabari wa kiafrika. Msikose kutumia fursa hii adimu ya kushiriki katika maonyesho haya ya kimataifa ambayo yana faida kubwa kwa wasanii, wanahabari, wanamitindo na makampuni (SMEs) na bidhaa zenu, nufaika kwa kujitangaza kimataifa.

No comments:

Post a Comment