T-PESA NA PBZ WASAINI KUSHIRIKIANA KIBIASHARA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 27 February 2019

T-PESA NA PBZ WASAINI KUSHIRIKIANA KIBIASHARA

Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa kwanza kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar kati ya pande zote mbili. 

Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini.  

Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakionesha nakala za mkataba wa makubaliano kufanya kazi kwa ushirikiano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini.  

Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano ya kufanya kazi kiushirikiano kibiashara. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte akiwa katika hafla hiyo.

Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa PBZ na TTCL (T PESA) walioshiriki katika hafla ya kuingia makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia kampuni yake tanzu ya T-PESA imesaini makubaliano ya kufanya kazi na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ambapo mawakala wa T-PESA watahudumiwa na benki hiyo.

Makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara kati ya PBZ na T-PESA yamefanyika leo mjini Zanzibar, ambapo Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce amesema yatawawezesha mawakala wao kupata huduma za kifedha kupitia PBZ.

Alisema T-PESA wanajivunia kufanikiwa katika ushirikiano huo kibiashara kwani utaiwezesha huduma zao kuenea kwa kasi zaidi, hasa ukizinga kuwa PBZ ni taasisi kubwa ya kifedha inayotoa huduma Zanzibar, Pemba na hata Tanzania Bara.

Miongoni mwa maeneo ambayo yamo katika mkataba wa ushirikiano huo kibiashara, mbali na PBZ kutoa huduma kwa mawakala wa T-PESA ya kutoa na kupokea fedha pia itakuwa ikitumia sehemu ya huduma za TTCL kama huduma za sauti na vifurushi, pamoja na huduma za simu.

Kwa upande wake,  Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte alisema benki hiyo inamtawanyiko mkubwa wa matawi yake kuanzia mjini na vijijini huku wakiwa na uzoefu mkubwa katika kutoa huduma za fedha kupitia simu za viganjani.

Kupitia mtawanyiko huo mkubwa kihuduma, tunapenda kuwahakikishia ushirikiano mzuri katika makubaliano hayo na jamii kwa ujumla watanufaika na kufurahia huduma zetu.

Aidha aliongeza kuwa Benki ya PBZ ni moja ya taasisi za fedha kongwe nchini Tanzania, ambayo inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). PBZ inalimiliki soko kwa takribani asilimia 50 huku ikiwa na wateja zaidi ya milioni 1.0.

No comments:

Post a Comment