Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, (wapili kulia), akipatiwa maelezo wakati akikagua mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme wa gesi asilia cha Somanga, Mkoani Lindi Februari 24, 2019. |
NA
SAMIA CHANDE, KILWA
NAIBU
Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu amekerwa na kasi ya mkandarasi State Grid katika kutekeleza miradi ya
kusambaza umeme vijijini Mkoani Lindi. Akizungumza
mwanzoni mwa ziara yake ya siku nne kukagua maendeleo ya usambazaji umeme
vijijini huko Wilayani Kilwa Mkoani Lindi Februari 24, 2019, Mhe. Mgalu alisema
kinachofanywa na mkandarasi huyo ni utapeli na ubabaishaji.
“Kiongozi
wao anakaa Ulaya, huku kaacha tu watendaji wengine yeye hayupo nchini, hili
halikubaliki kwani wanakwamisha juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli za kuhakikisha wananchi wote wa Tanzania
wanapata umeme wakiwemo wa vijijini.” Alisema.
Alisema,
Wakandarasi wanaofanya kazi ya kusambaza umeme vijijini wamekabidhiwa kwa Wakuu
wa wilaya na kuwataka wakuu wa wilaya kuchukua hatua kali dhidi ya wakandarasi
wote wanaokwenda kinyume na mikataba yao kwa kufanya kazi kwa kusuasua bila
sababu zozote za msingi.
Akionyesha
kukerwa na kutoridhishwa na ubora wa kazi iliyofanywa na mkandarasi huyo yaani State Grid, Mhe. Naibu Waziri aligoma
kuwasha umeme katika vijiji vya Nangambi na Naipul Kata ya Mingumbi Wilayani Kilwa
na kuwataka wananchi kuwa na uvumilivu kwani suala la mkandarasi huyo atalifikisha kwenye mamlaka
zinazohusika ili hatua za haraka zichukuliwe na ikiwezekana kuleta mkandarasi mwingine akamilishe kazi hiyo.
Pia Naibu
Waziri alipata fursa ya kutembelea kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi
asili cha Somanga, (Somanga gas plant)
kilichopo Somanga Fungu nakujione matengenezo ya mashine yanavyoendelea.
Kwa
mujibu wa Meneja wa kituo hicho, Mhandisi Oscar Kidia, alimueleza Mhe Naibu Waziri kuwa kwa sasa mashine mbili katika
kituo hicho zenye uwezo wa kutoa Megawati 5 zimefanyiwa matengenezo.
Nia
ya Serikali ya awamu ya Tano ni kupeleka umeme wa uhakika na wakutosha katika
Mikoa ya Kusini hivyo wananchi wawe tayari kuupoke umeme unapofika katika miji
na vijiji kwani umeme utawasaidia kuchoche maendeleo na kukuza shughuli za kiuchumi
katika maeneo yao.
Wananchi wa Nangambi na Naipul kata ya Migumbi Wilayani Kilwa wakimsikiliza Naibu wazi Wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (hayupo pichani) wakati akiwahutubia.
No comments:
Post a Comment