Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Kampuni ya Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. |
Viongozi mbalimbali na wananchi wameendelea kutuma salamu za rambirambi na kumiminika nyumbani kwa wazazi wa marehemu Ruge unapofanyika msiba huo. Jana mara baada ya kutokea kwa taarifa za kifo chake, Rais Dk. John Pombe Magufuli alitoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kupitia ukurasa wake wa twita akionesha majonzi yake nakuungana na wanafamilia.
Wengine walioendelea kutoa salamu za pole huku wakionesha kuguswa na msiba huo, ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Acson na mawaziri na viongozi mbalimbali.
Rais Magufuli aliandika; "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana. Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina."
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliandika:
"Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu."
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan ameandika;
"Umewafungulia Dunia mamia ya Vijana nchini, umekuwa mbunifu na mtambuzi wa fursa mbalimbali, Hakika tumepoteza Shujaa na Mpiganaji mahiri. Pumzika kwa amani Ruge."
Tutaendelea kuwafahamisha kinachojiri katika msiba huu mkubwa kwa tasnia ya Habari na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya kauli za viongozi kwenye mitandao ya kijamii;
Mwigulu Nchemba: "Umeondoka Ruge Mtahaba, Umeondoka Shujaa, Umeondoka Mpambanaji. Pole kwa familia,ndugu na Jamaaa, Pole zaidi kwa watanzania wote kwa msiba huu mzito. "Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika" Ayubu 42:2, Amen"
Reginald Mengi: "RIP Ruge Mutahaba. The Media fraternity is shocked by the very sad news of your untimely departure. You leave behind a huge gap which we shall find very difficult to fill. You were truly a gentleman and pioneer in many aspects of the media. Farewell our Brother."
No comments:
Post a Comment