MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AMPONGEZA MBUNGE WA USHETU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 12 February 2019

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AMPONGEZA MBUNGE WA USHETU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwa Katibu wa chama hicho kwa mkoa wa Shinyanga, Bi. Haula Kachambwa, wilayani Kahama, jana.


Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (wa pili kulia), akicheza ngoma mara baada ya kumpokea Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (hayupo pichani), alipowasili katika shule ya Sekondari ya Dakama, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga jana.



Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akikabidhi pikipiki mbili kwa Jeshi la Polisi wa Halmashauri ya Ushetu kwa ajili ya shughuli za ulinzi na usalama wa wananchi.

MAKAMU wa Pili Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amempongeza Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kwa kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapunduzi (CCM), katika kipindi cha miaka mitatu kwa vitendo.

 Makamu wa Pili wa Rais ametoa pongezi hizo alipowasili katika jimbo la Ushetu, wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga na kuzungumza na wajumbe wa kata 20 ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wana CCM kutembea kifua mbele kwa kuzungumzia mafanikio yaliyotokana na chama hicho.

 Aidha, amewataka uongozi wa CCM mkoa kuwa na umoja na kushirikiana katika kutekeleza ilani na kuepusha migogoro itakayopelekea CCM kugawanyika. "Chama cha Mapinduzi kimefanya mambo mazuri mengi kwa wananchi hivyo hakikisheni mnayasema, msiposema nyie, mtasemewa na wapinga maendeleo", amesisitiza Makamu wa Pili wa Rais.

 Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2015 hadi 2018, Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Elias Kwandikwa, ameemueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa kwa ushirikiano na wananchi wa jimbo lake katika sekta ya elimu wamefanikiwa kujenga madarasa 40 katika shule za Sekondari, matundu ya vyoo 109 na madawati 1015.

 Katika Sekta ya Afya, Mbunge huyo, ameeleza kuwa Halmashauri ya Ushetu imefanikiwa kuwa na vituo 3 vya Afya na ujenzi umeanza wa Hospitali ya Wilaya ambayo inategemewa kukamilika ifikapo Juni, 2019 Sambamba na hilo amejenga zahanati 22 kutoka zahanati 17 zilizokuwepo awali ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 22 kufikia Desemba 2018.

 Katika Sekta ya Maji ameeleza kuwa amejenga miundombinu ya maji mpya na kukarabati visima vya maji 113 vilivyopo, kuunda na kusajili Jumuiya za watumiaji maji na kutafuta vyanzo vipya vya maji kwa kuchimba visima virefu 11 kwa vijiji kame.

 Katika hatua nyingine, Mbunge huyo jana ametoa vyereheni 20 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT), pikipiki 2 na printa kwa Jeshi la Polisi la halmsahauri yake na kompyuta za mezan 20 kwa Shule ya Sekondari ya Dakama, kama mchango wake katika kusaidia wananchi wa jimbo lake.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Shinyanga yupo katika ziara ya kikazi ya Chama ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

No comments:

Post a Comment