Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel, 'Royal Bundle' na 'Tomato Bundle' uliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Dar Es Salaam leo. |
Sehemu ya wageni maarufu wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma mpya za Halotel, 'Royal Bundle' na 'Tomato Bundle' uliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Dar Es Salaam leo. |
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Halotel imezinduwa huduma kabambe ya 'Royal Bundle' ambayo inawawezesha wateja wake kupata huduma hiyo bila kikomo kama vile kupiga simu za ndani na hata kimataifa pasipo kikomo.
Huduma hiyo pia itamwezesha mtumiaji kutumia intaneti bila kikomo pamoja na kuunganishwa moja kwa moja pindi vifurushi vyao vinapokuwa vimekwisha bila wao kurudia kujiunga tena.
Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania, Nauyen Van Trung alisema mbali na kuzingatia unafuu na huduma zao, ubunifu ni silaha kubwa ambayo wamekuwa wakiitegemea katika kuwafikia wateja wa makundi yote kila kona nchini.
"Ninayo furaha kubwa kuwatangazia ujio wa huduma hii kabambe ambayo tunategemea italeta mapinduzi makubwa nchini katika mawasiliano. 'Royal Bundle' imekuja kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatamani kutumia huduma zetu bila ya kupata bugudha ya aina yoyote zikiwemo salio kuisha au intaneti kukata," Bw. Trung.
"Halotel tunatambua umuhimu wa sekta ya mawasiliano katika shughuli za kiuchumi hivyo tusingependa kampuni yetu kuwa kikwazo katika kulifanikisha hilo. Ndio maana leo tunawatangazia Watanzania wote kuwa kwa shilingi 10,000 tu unaweza kupiga simu za ndani na kimataifa kama vile kwenda nchi za India, China, Canada na Marekani bila ya kikomo, kutumia intaneti bila kikomo, kutumia sms bila kikomo na kama haitoshi mara tu muda wa kifurushi utakapo kwisha tutakuunganisha mara kwa mara," alisema Bw. Trung.
Aidha sambamba na hayo, Bw. Trung alizinduwa pia huduma nyingine ijulikanayo kama 'Tomato Bundle' ambayo ni maalum kwa wateja wa Halotel nchi nzima, itakayomwezesha mteja kupiga simu bure kwenda namba yoyote ya Halotel kwa dakika 5 za mwanzo kwa kila simu pamoja na kupata salio la ziada la bure la sh4000 ambalo mteja atalitumia kwenye huduma nyingine za Halotel (kwa mwezi mzima).
"...Ili mteja aweze kufurahia huduma hii (Tomato Bundle) anapaswa kuwa na laini ya Haloteli ya Tomato ambayo itanunuliwa kwa sh8000 tu laini hiyo itamuwezesha kupiga simu kwa kila namba yoyote ya Halotel bure kwa dakika 5 za mwanzo, licha ya hapo mteja atapata salio la ziada la shs4000 bure ambalo atalitumia kwenye huduma nyingine apendazo za Halotel," aliongeza Naibu Mkurugenzi, Bw. Trung.
No comments:
Post a Comment