WASANII NANDY, JUMA NATURE, SHOLO MWAMBA KUONGOZA HALOTEL SHUKRANI CONCERT, MBAGALA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 4 January 2019

WASANII NANDY, JUMA NATURE, SHOLO MWAMBA KUONGOZA HALOTEL SHUKRANI CONCERT, MBAGALA

Msanii maarufu wa miondoko ya kisingeli, Sholo Mwamba akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) alivyojiandaa kuwaburudisha wateja wa Halotel watakaojitokeza kesho kwenye tamasha la ‘Halotel Shukrani Music Concert’ litakalofanyika Mbagala viwanja vya Zakiem.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Mhina Semwenda akizungumzia tamasha la ‘Halotel Shukrani Music Concert’ litakalofanyika kesho tarehe 5, Mbagala viwanja vya Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Nong Thi Lien, Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel.

Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Bi. Nong Thi Lien akizungumzia tamasha hilo kwa wanahabari leo. 

Mratibu wa Tamasha hilo, Rehema Jonas akizungumza.

Msanii Jolie akijinasibu alivyojipanga.

Msanii Gigy Money ndani ya nyumba pia kesho.

Msanii Benson akizungumza na wanahabari. 

Kutoka kushoto ni wasanii Sholo Mwamba, Jolie, Benson pamoja na Gigy Money...


WASANII maarufu Juma Nature, Nandy, Sholo Mwamba, Gigy Money, Jolie, J. Melody pamoja na Benson wamejiandaa vikali kutoa burudani kabambe katika tamasha kubwa la Shukrani kwa wateja lililoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel Tanzania.

Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Bi. Nong Thi Lien amesema tamasha hilo la muziki limeandaliwa kutoa shukrani kwa wateja wao kwa kuwaunga mkono.

Amesema tamasha hilo litakalofanyika kesho katika viwanja vya Mbagala Zakiem kuanzia saa sita mchana litapambwa na wasanii mbalimbali, wakiwemo Juma Nature, Nandy, Sholo Mwamba, Gigy Money, Jolie, J. Melody pamoja na Benson.

Wakizungumza na wanahabari leo wasanii hao walisema wamejiandaa vema kutoa burudani ya kufa mtu na wateja wa halotel, hivyo kuwataka wakazi wa Dar es Salaam hasa Temeke kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hizo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel, Mhina Semwenda alisema tamasha la muziki kuwashukuru wateja litaendelea maeneo mbalimbali huku likiambatana na kusaidia jamii masuala anuai ya kijamii.

“…Tunaomba wakazi wa Temeke tujumuike pamoja kwe ‘Halotel Shukrani Music Concert’ pale  Mbagala Zakiem kushuhudia burudani kabambe utakayotolewa na wasanii kibao,” alisema.

No comments:

Post a Comment