RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL IKULU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 11 January 2019

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA BHARTI AIRTEL IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma taarifa ya majadiliano kutoka kwa mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya Mazungumzo yao . Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel aliyeambatana na ujumbe wake kutoka kampuni ya Simu ya Airtel pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba John Kabudi, Gavana wa BOT Profesa Luoga, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James, Mtendaji mkuu wa kituo cha Uwekezaji (TIC ) Geoffrey Mwambe  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL  Mhandisi Omary Nundu. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Bw. Sunil Mittal Mwenyekiti wa Bharti Airtel  ( kampuni ya Simu ya Airtel ) mara baada ya kuwasili kwaajili ya mazungumzo , Ikulu Jijini Dar es Salaam. Januari 11,2019.

No comments:

Post a Comment