NAIBU WAZIRI KANYASU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 10 January 2019

NAIBU WAZIRI KANYASU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA TANZANIA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (kulia) akizungumza naBalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke  (katikati) mapema leo akiwa  na ujumbe wake,  wakati alipomtembelea ofisini kwake Mpingo House  jijini Dar es Salaam.

BALOZI wa Uingereza Tanzania, Sarah Cooke mapema leo Alhamisi Januari 10, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Mpingo House jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kukabiliana na tatizo la ujangili wa tembo pamoja na mikakati ya kukuza  utalii nchini.

No comments:

Post a Comment