Wakipeana mkono ikiwa ishara ya kufurahia kukutana na watoto yatima. |
wakiwabeba watoto yatima. |
KAMPUNI Ya usafirishaji abiria ya Moovn Driver kwa kushirikiana na umoja wa madereva wa mtandao (TODA), leo wametoa msaada wa vyakula na mavazi kwa kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Hananasifu, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu wa Umoja wa Madereva wa Mtandao (TODA), Fredy Peter, amesema kuwa msaada huo umelenga kuwapatia nafuu katika mazingira waliyomo na akatoa wito kwa makampuni na taasisi zingine ziige mfano huo kuwasaidia watu wenye mahitaji, hasa watoto wanaoishi kwenye vituo vya mayatima.
No comments:
Post a Comment