Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi,
Mhe. Elias John Kwandikwa akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi
Iponyanholo alipokwenda kukagua miundombinu ya shule hiyo.
Walimu na wazazi wa shule ya msingi Songambele
katika Jimbo la Ushetu Wilayani Kahama wakimsikiliza Mbunge wao ambaye ni Naibu
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (hayupo pichani), alipokwenda
kukagua maendeleo ya shule hiyo.
Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo alipokutana na Walimu na
Wazazi wa shule ya msingi Songambele alipokagua maendeleo ya shule hiyo.
Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akifurahia kukamilika kwa vitanda 22,
alivyovikabidhi kwa shule ya Sekondari Bulungwa ili kuwawezesha wasichana wa
shule hiyo kusoma bweni badala ya kutwa.
Mbunge wa Ushetu ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akizungumza na wazee wa kijiji cha Bukale
mara baada ya kuwalipia Bima ya Afya ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi
katika jimbo hilo kujiunga na bima ya afya.
MBUNGE
wa Ushetu ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa
amezungumzia umuhimu wa viongozi, walimu na wazazi katika jimbo hilo
kuunganisha nguvu ili kuongeza ufaulu na kuondoa division zero.
Akizungumza katika
ziara yake ya kukagua utekelezaji wa huduma za maji, elimu, afya na miundombinu
katika jimbo hilo amesisitiza kila mwanajamii wa jimbo hilo kuhakikisha elimu
inaimarika ili fursa nyingine ziweze kufanikiwa.
“Ndugu zangu
tukifanikiwa katika elimu, miradi mingine ya maji, kilimo, afya na miundombinu
itafanikiwa na uchumi wa jimbo hili utakuwa kwa kasi amesisitiza”, Mhe.
Kwandikwa.
Katika ziara hiyo Mbunge
huyo amekabidhi vitanda 22 kwa shule ya Sekondari ya Bulungwa kwaajili ya
mabweni ya wasichana ili kuwawezesha wanafunzi wengi kusoma bweni badala ya
kutwa.
Amemtaka Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Ushetu Bw, Michael Matomola kuhakikisha shule zinazostahili kuwa
na maabara katika jimbo hilo ikiwemo Sekondari ya Sabasabini inakuwa na huduma
hiyo haraka ili kuwezesha wanafunzi kufaulu masomo ya sayansi.
Amewataka viongozi, wazazi
na walimu kubaini vipaumbele vinavyotekelezeka kwa haraka ili kuleta mabadiliko
chanya katika jimbo hilo. Mbunge huyo wa Ushetu
ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John alikuwa katika ziara ya siku
mbili jimboni humo kukagua na kuhamasisha maendeleo ya elimu, maji, afya, kilimo
na miundombinu katika jimbo la Ushetu Wilayani Kahama.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
No comments:
Post a Comment