RAIS DK MAGUFULI AWAAPISHA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA SKAUTI MKUU TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 4 October 2018

RAIS DK MAGUFULI AWAAPISHA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA SKAUTI MKUU TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza muda mfupi baada ya kumuapisha kuwa Skauti Mkuu wa Chama Cha Skauti Tanzania. Aliyeketi ni Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe aliyemuapisha kuwa Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hafla hii imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi na Skauti Mkuu Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama  baada ya kuwaapisha Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu Bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 20 Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2018 Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment