Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu (kulia), akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na leo kabla ya kusaini mkataba wa upimaji utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu kabla ya kusaini mkataba wa upimaji utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu kabla ya kusaini mkataba wa upimaji utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mwanasheria Mkuu wa MSD, Christopher Kamugisha.
Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa(MSD) Laurean Rugambwa Bwanakunu leo wamesaini mkataba wa upimaji utendaji kazi wa Mkurugenzi huyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Bwanakunu amesaini mkataba huo mbele ya Menejimenti ya MSD.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Dkt. Ulisubisya amewapongeza MSD kwa kuteuliwa kuwa mnunuzi Mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ameagiza pia mikataba ya kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka kwa wazalishaji iangaliwe na kuandaliwa vizuri hasa wakati huu ambao MSD inahitaji shehena kubwa kwa ajili ya kuhudumia nchi 16 wanachama wa SADC.
Kabla ya kusaini mkataba huo, Bwanakunu alimueleza Katibu Mkuu mafanikio ya malengo matano aliyojiwekea mwaka wa fedha uliopita, ikiwa ni pamoja kuimarisha uwezo wa kifedha, kuboresha mifumo ya Tehama, kushirikisha wadau,kuboresha tija ya wafanyakazi mahali pa kazi,pamoja kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara, ambapo amefanikisha kwa 96%.
No comments:
Post a Comment