NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Saturday, 8 September 2018

NAIBU WAZIRI UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI TANZANIA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu waliofanya vizuri katika masomo ya uhandisi alipokuwa akifunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa akizungumza na wahandisi kabla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa (kulia) akimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wahitimu wa vyuo vikuu waliofanya vizuri katika masomo ya uhandisi alipokuwa akifunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018.

Baadhi ya wahandisi wapya wakila kiapo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma, utii na uzalendo kabla ya kukabidhiwa leseni zao kwenye hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018. Jumla ya wahandisi 430 walikula kiapo hicho mbele ya kamishna wa viapo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa.

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (wa tatu kushoto) pamoja na meza kuu wakishudia zoezi la kiapo kwa wahandisi wapya. 

Ofisa wa viapo wa Serikali na Hakimu Mkazi Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Wanjaha Hamza akisimamia zoezi la viapo kwa wahandisi wapya.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (hayupo pichani)

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania, Eng. Profesa Ninatubu Lema katika sherehe hizo.

Baadhi ya wahandisi wapya wakila kiapo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma, utii na uzalendo kabla ya kukabidhiwa leseni zao kwenye hafla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018. Jumla ya wahandisi 430 walikula kiapo hicho mbele ya kamishna wa viapo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa (katikati) akimkabidhi leseni mmoja wa wahandisi wapya mara baada ya kiapo cha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taaluma, utii na uzalendo kabla ya kufunga rasmi Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi Tanzania 2018. Jumla ya wahandisi 430 walikula kiapo hicho mbele ya kamishna wa viapo wa Serikali 

No comments:

Post a Comment