MASHIRIKA YATAKIWA KUHUDUMIA JAMII KWA KUREJESHA FAIDA WANAYOPATA - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 28 September 2018

MASHIRIKA YATAKIWA KUHUDUMIA JAMII KWA KUREJESHA FAIDA WANAYOPATA

Mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA, Julias Konyani akikabidhi Hundi kutoka Benki ya CBA kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Ufundi na Msingi Sing'isi. anayeshudia ni Mkuu wa Shule hiyo, Safira Ndelwa wakati wa makabidhiano ya hundi. Picha na Ahmed Mahmoud.

Na Ahmed Mahmoud Arusha

TAASISI na mashirika mbali mbali hapa nchini yametakiwa kurudisha sehemu ya faida wanayo ipata ili kuhudumia Huduma za kijamii zikiwemo Mausala ya afya elimu na watoto wasiojiweza Sanjari na maafa mbali mbali. Akizungumza wakati akitoa msaada kwenye shule ya Msingi na ufundi Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha mkuu wa idara ya wateja masoko na mawasiliano wa Benki ya CBA bwana Julias Konyani amesema kwamba katika faida wanayo ipata watakikisha wanaendelea kusaidia sekta ya elimu nchini

Aidha ameyataka mashirika mbali mbali kuona namna ya kurudisha faida wanayopta katika kuhudumia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kusaidiana na serikali katika hatua mbalimbali za kuwaleta maendeleo wananchi hususani benki hiyo ilipokuwa ikikabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni 4 katika shule ya msingi na ufundi ya Sing’isi.

Amezitaka taasisi mbali mbali kujitokeza katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bure na kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya awali bila kuwepo na changamoto ya madarasa pamoja na uhaba wa vitabu vya kiada na ziada kwa ajili ya kusoma na kufundishia.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Singisi Safira Ndelwa ametaja changamoto mbali mbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni uchakavu wa miundo mbinu ya majengo katika shule hiyo ikiwemo uhaba wa vyumba vya kusomea na uzio wa shule.

"Shule hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uzio uhaba wa vyumba vya madarasa mashine ya kuchapisha mitihani pamoja na nyumba za walimu," alisema mwalimu Ndelwa.

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Anjela Izack ameshukuru benki hiyo kwa msaada huo na kuomba kuongezewa madarasa mawili kwa lengo la kuondoa usumbufu wa wanafunzi wenzake kusoma kwa awamu mbili kwani wanachoka na masomo yao na kujikuta wakishindwa kushika masomo na maendeleo kushuka.

No comments:

Post a Comment