MWILI wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana. Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maofisa wengine wa Umoja wa Mataifa.
Kiongozi huyo, anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi. Kulikuwa na hali ya maombolezo wakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi. Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima. Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia. -BBC
Gabon kufanya uchaguzi wa rais Aprili 12
-
Hatimaye Serikali ya mpito ya Gabon ilisema uchaguzi wa rais utafanyika
Aprili 12, hatua muhimu ya kurejesha utawala wa kiraia baada ya mapinduzi
yaliyom...
NOTI MPYA KUANZA KUTUMIKA TAREHE 1 FEBRUARI, 2025
-
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea
Noti Mpya kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, elfu Mbili na shilingi
elfu ...
No comments:
Post a Comment